• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Morogoro District Council
Morogoro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Afya
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Utalii
    • Vivutio vya Utalii
      • Msitu wa Pangawe
      • Msitu wa Milawilila
      • Msitu wa Kimboza
      • Maji Moto-Kisaki
      • Kisimbi-Kinole
      • Utalii Matombo
    • Maeneo ya Kihistoria
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Huduma za Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WAKURUGENZI MOROGORO WATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA IFIKAPO JANUARI MWAKANI

Imetolewa: December 26th, 2018

Na. Andrew Chimesela - Morogoro.

Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoa wa Morogoro wametakiwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule yakiwemo madarasa kabla au ifikapo Januari 28 mwakani ili kuwafanya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuwa na mazingira bora ya kusomea.

Hayo yamefahamika wakati wa kikao cha Uchaguzi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na Kidato cha kwanza Januari 2019 kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Morogoro ambacho pia kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Elimu.

Muda mfupi kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Ernest Mkongo alisema wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani mwaka huu walikuwa 48,301 lakini waliofanya mtihani ni 47,961 sawa na asilimi 99.

Kwa mantiki hiyo, Kaimu Katibu Tawala huyo wa Mkoa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mali ameagiza kila Halmashauri ndani ya Mkoa wa Morogoro kwenda kutathmini  matokeo hayo na kupanga mikakati ya kuwapokea wanafunzi hao na kuwatayarishia mazingira ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa madarasa.

Amesema ifikapo Januari 28, 2019 majengo yote ya shule za Sekondari yanayojengwa  au kukarabatiwa kwa kila Halmashauri Mkoani humo yawe yamekamilika bila visingizio vyovyote, lengo ni kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na wanafunzi waliofaulu ambao hawataripoti wazazi wao wachukuliwe hatua za kisheria.

“Hatutapokea visingizio vya aina yoyote kwa wanafunzi wasioripoti shuleni, hatua za kisheria zichukuliwe kwa wazazi au walezi watakaokwamisha wanafunzi hawa kuendelea na masomo yao” alisema Bw. Mkongo.

Naye Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. George Jidamva pamoja na kuupongeza Mkoa kwa kuwa na ufaulu mzuri ameagiza kuwasimamia Waratibu wa Elimu ngazi ya Kata kusimamia vema majukumu yao ili Mkoa uendelee kupata ufaulu mzuri zaidi .

Amesema kwa sasa Watendaji hao hawana kisingizio chochote kwa kuwa Serikali imekwisha wapatia usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kuwasaidia kusimamia vema majukumu yao hivyo ni vema watendaji hao wakatumia vema usafiri waliopewa kwa manufaa ya kazi zao na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo Dkt. Jidamva  amekumbusha kuendelea kusimamia uwepo wa chakula cha wanafunzi shuleni, kukamilisha ujenzi wa madarasa yatakayopelekea wanafunzi kupata masomo yao katika mazingira yaliyobora.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joyce Baravuga amebainisha kuwa  Mkoa wa Morogoro umepanda ufaulu kwa asilimia 6.6 ambapo mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 70.78 na mwaka huu ufaulu umepanda hadi kufikia  77.38 wastani huo unatokana na kupanda kwa ufaulu kwa Halmashauri 8 kati ya 9 za Mkoa wa Morogoro ambapo Halmashauri moja tu ya Gairo ndiyo iliyoshuka kwa ufaulu kwa asilimia 5.73.

Mkoa wa Morogoro umefanikiwa kutoa mwanafunzi wa pili kitaifa INNOCENT PAUL SELELI kutoka shule ya Msingi Carmel katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na hivyo mwanafunzi huyo kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 10, 2025
  • TANGAZO A UPANGA VYUMBA VYA OFISI NA MAENEO MBALIMBALI YALIYOPO MOROGORO MJINI March 19, 2025
  • TANGAZO LA KAZI May 23, 2022
  • ORODHA YA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI 2018. September 07, 2018
  • Angalia zote

Habari za hivi karibuni

  • SHILINGI MILIONI 538 NA LAKI NNE KUNUFAISHA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WALEMAVU

    June 20, 2025
  • MAAFISA HABARI HAKIKISHENI WANANCHI WANAPATA HABARI SAHIHI: MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • KIONGOZI MBIO ZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI ILIYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 12, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEEA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO,MAAGIZO YATOLEWA

    April 11, 2025
  • Angalia zote

Video

Mfumo wa Mikopo ya 10% Namna ya Kujisajili
Vidio Zaidi

Kurasa za haraka

  • Sheria ya Manunuzi ya umma
  • Sheria ya Ardhi

Tovuti nyingine

  • Salary Slip Self Service
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani yake

Wasiliana nasi

    Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road

    Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania

    Simu: +255 23 2935458

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.