Mhe Omary Mgumba (Mbunge) Mnaibu waziri wa Kilimo akiwa katika Ziara ya siku sita Jimboni kwake Morogoro Kusini Mashariki Tangu Tarehe 01/01/2019 Mpaka Tarehe 06/01/2019.
Lengo la ziara hiyo ni Kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Raisi Dr John Joseph Pombe Magufuli katika jimbo hilo Pamoja na kuhamasiha wananchi Kujitolea katika ujenzi wa miundombinu ya Vyumba vya Madarasa kufuatia ufaulu Mkubwa wa watoto wanaotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mwezi huu wa kwanza na kusikiliza shida, Kero na Changamoto zinazowakabili wananchi wenzake anaowawakilisha ili kwa kushirikiana nao Pamoja na Serikali yao kuzipatia ufumbuzi.
Mafanikio ya ufaulu mzuri wa wanafunzi umeleta changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 17 katika kata Saba kwenye tarafa za Mkuyuni na Ngerengere. shule hizo Mkuyuni Vyumba 7, Kinole 2, Kiroka 2, na Tomondo 3 kwenye tarafa ya Mkuyuni na Ngerengere Vyumba 3, Kidugalo 2 na Tununguo 1.
Pia katika ziara hiyo Mhe Mgumba amepata fursa ya Kutembelea Kituo cha Afya Mkuyuni kujionea hali ya ujenzi unavyoendelea .
Pichani Mhe Mgumba akiwa na Mhr Diwani wa kata hiyo Mhe Mwinyi Buyi na viongozi wengine wakikagua hali ya ujenzi huo.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.