MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halamshauri zote zilizopo Mkoa wa Morogoro kutoa elimu ya kutosha ya Bima ya CHF iliyoboreshwa (iCHF) kwa Wananchi.
Hayo ameyazungumza Julai 16, 2021 katika Mkutano wa Nusu Mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa Lishe na Bima ya Afya ya Jamii (ICHF).
Akizungumza na waashiriki katika Mkutano huo, RC Shigela, amesema zipo changamoto katika Mkoa wa Morogoro kwenye muitikio wa Wananchi kukata Bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa .
RC Shigela, amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuona njia mbalimbali za kuongeza idadi ya wananchi katika mfuko wa bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.
Amesema kwa Mkoa wa Morogoro umefikia asilimia 9.4 ya zoezi la uandikishaji wa Bima za CHF iliyoboreshwa ambapo kwa malengo ya kufikia mwaka 2025 Mkoa wa Morogoro unatakiwa kufikia asilimia 34%.
Amesema kuwa kati ya asiliia 9.4% za waliojiandikisha katika mfuko wa Bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa ni asilimia 3.4% ya wananchi ambao ndio wanapata huduma ya bima ipasavyo.
‘’Bado Mkoa wetu wa Morogoro tunachangamoto kubwa ya bima hii ya CHF iliyoboreshwa , asilimia ya wanachama wetu tuliowaandikisha hawapati huduma kama inavyostahili, kumekuwa na malalamiko sana katika upande huu wa bima, wengi wanalalamika dawa hakuna wakati sehemu nyengine zipo, Maafisa Maendeleo nyie ni watu muhimu sana katika eneo hili, na muna jukumu hilo na ndio maana mmesomeshwa na Serikali tupe huo utaalamu hakikisheni idadi ya wanachama wanaongezeka’’Amesema RC Shigela.
Katika hatua nyengine, amepiga marufuku Watumishi katika Vituo vya afya wanaotumia fedha za huduma zinazotolewa na wagonjwa Hospitalini kuzifanya ni mali yao.
Amesema kuwa Katika Vituo vya afya kumekuwa na mchezo mchafu ambao baadhi ya watumishi wamekuwa wakihudumia wagonjwa wasiokuwa na bima kuchukua fedha bila kuingiza katika mfumo wa malipo.
‘’Nitoe rai kwa waatumishi wa namna hiyo , utakuta baaadhi ya Vituo vya afya idadi kubwa ya wanaohudumiwa wamekuwa wakiwaandikisha katika matibabu ya huduma za msamaha , huku fedhaa za wagonjwa wakizitumbukiza mifukoni , tutakao wabaini tutachukua hatua kubwa za kisheria , ni bora tubakie na watumishi wachache kuliko kubaki na rundo la watumishi wanaotuhujumu’’Ameongeza RC Shigela.
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja, amewaomba wataalamu pamoja na wadau wa afya wasirudi nyuma kwani suala la lishe linatakiwa lipewe kipaumbele.
Bi. Mtunguja, amesema kuwa tofauti kubwaa ya watoto kupishana kiakili kinatokana na kupata lishe bora.
‘’Mtoto akipata virutubisho vya kutosha anakuwa na akili nyingi, sasa ni jukumu letu kuhakikisha suala la lishe linakuwa agenda mama katika vikao vyetu ili tutengeneze vizazi vyenye akili kwa ajili ya Mkoa wetu wa Morogoro na Taifa kwa ujumla’’ Amesema Bi. Mtunguja.
Amesema kuanzia mwaka wa fedha wa 2021/2022 vipimo vya utambuzi wa lishe vitaapimwa kuanzia ngazi ya Kata.
Katika Mkutano wa nusu mwaka wa Tathimini ya Mkataba wa Lishe na Bima ya afya ya Jamii (iCHF) , umehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wataalamu wa Halmashauri, Wataaalamu wa Lishe ngazi ya Mkoa na Halmashauri pamoja na wadau wa lishe Mkoa na Halaamshauri zote.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.