• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Morogoro District Council
Morogoro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Afya
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Utalii
    • Vivutio vya Utalii
      • Msitu wa Pangawe
      • Msitu wa Milawilila
      • Msitu wa Kimboza
      • Maji Moto-Kisaki
      • Kisimbi-Kinole
      • Utalii Matombo
    • Maeneo ya Kihistoria
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Huduma za Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

"BAINISHENI VYANZO VYA MAJI NA MVILINDE" MHE.KASSIM MAJALIWA MAJALIWA

Imetolewa: March 5th, 2025

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), amezitaka Mamlaka za Serikali za Mikoa na Wilaya kuhakikisha zinabainisha vyanzo vya maji, kushirikisha wananchi wanaoishi karibu na vyanzo hivyo, na kuvipa ulinzi kwa kutunga sheria ndogo za kulinda vyanzo hivyo ili kuondokana na uharibifu wa vyanzo hivyo.

Agizo hilo limetolewa Machi 5, 2025, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bwawa la Kidunda, lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani humo ujenzi unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga.

Mhe. Majaliwa amesema ipo haja ya mamlaka hizo kutambua vyanzo vya maji katika maeneo yao ili kuweka mikakati ya kuvilinda na kuzuia uharibifu wa vyanzo hivyo kwa maslahi mapana ya Taifa na kusisitiza Mamlaka za Maji kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na kuwataka wakulima na wafugaji kuendelea kufanya shughuli zao pasipo kuathiri vyanzo hivyo.

"Nazitaka Mamlaka za Mikoa na Wilaya zifanye kazi ya kubainisha vyanzo vyote muhimu vinavyotiririsha maji na kutuletea maji kwenye maeneo yetu," amesisitiza Mhe. Kassim Majaliwa.



Sanjari na hayo, Waziri Mkuu amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa bwawa la kidunda kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kwa viwango vya ubora vinavyotakiwa huku akiwataka wananchi wanaozunguka mradi huo kuwa walinzi namba moja wa vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa bwawa hilo ili kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu.



Katika hatua nyingine, Mhe. Majaliwa amewataka wananchi wa mkoa wa Morogoro kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuishi huku wakiheshimiana kwa kuwa wote wanategemeana na kukemea tabia ya baadhi ya wafugaji kulisha mifugo yao mashamba ya wakulima na kwamba  jambo hilo kamwe halikubaliki.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, amesema lengo la Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama, Hivyo ameitaka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kutosubiri kukamilika kwa ujenzi wa bwawa hilo la Kidunda na kutoa wiki moja timu ya mamlaka hiyo iende Tarafa ya Ngerengere kuhakikisha wanatafuta maji kwa ajili ya wananchi wa Tarafa hiyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, akitoa Salam za Mkoa amesema, hadi Februari 2025, wastani wa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Morogoro ni takribani 70% huku akibainisha kuwa Mkoa huo una miradi ya maji ya RUWASA yenye thamani ya shilingi bilioni 90, miradi ya maji ya MORUWASA ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 20, na miradi mingine ina thamani ya shilingi bilioni 75 na kwamba hiyo yote ni jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kumtua mwanamke ndoo kichwani.

Ujenzi wa Bwawa la Kidunda ambao kwa sasa umefikia 28% hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 335, na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu na unatarajiwa kukamilika Disemba 2026. Mradi huo unatekelezwa na Serikali Kuu kupitia Wizara ya Maji na kusimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO A UPANGA VYUMBA VYA OFISI NA MAENEO MBALIMBALI YALIYOPO MOROGORO MJINI March 19, 2025
  • TANGAZO LA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU, DEREVA NA MTENDAJI WA KIJIJI July 15, 2024
  • TANGAZO LA RASIMU July 25, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi karibuni

  • KIONGOZI MBIO ZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI ILIYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 12, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEEA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO,MAAGIZO YATOLEWA

    April 11, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO AENDELEZA KAMPENI YA JISOMESHE NA MKARAFU

    March 14, 2025
  • "BAINISHENI VYANZO VYA MAJI NA MVILINDE" MHE.KASSIM MAJALIWA MAJALIWA

    March 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Mfumo wa Mikopo ya 10% Namna ya Kujisajili
Vidio Zaidi

Kurasa za haraka

  • Sheria ya Manunuzi ya umma
  • Sheria ya Ardhi

Tovuti nyingine

  • Salary Slip Self Service
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani yake

Wasiliana nasi

    Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road

    Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania

    Simu: +255 23 2935458

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.