• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Morogoro District Council
Morogoro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Afya
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Utalii
    • Vivutio vya Utalii
      • Msitu wa Pangawe
      • Msitu wa Milawilila
      • Msitu wa Kimboza
      • Maji Moto-Kisaki
      • Kisimbi-Kinole
      • Utalii Matombo
    • Maeneo ya Kihistoria
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Huduma za Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO AENDELEZA KAMPENI YA JISOMESHE NA MKARAFU

Imetolewa: March 14th, 2025



Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa ameendelea kuhamasisha kampeni ya "Jisomeshe na Mkarafuu" kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na wakazi wote wa Wilayani Mvomero, ikiwa na lengo la kuwawezesha wanafunzi hao kiuchumi kupitia kilimo cha mkarafuu na kujisomesha kupitia kilimo cha zao hilo.

Akizungumza wakati wa zoezi la kugawa miche hiyo kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari za Kipera na Homboza Machi 14, 2025 Dkt. Mussa amesema Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameanzisha kampeni hiyo kama mkakati wa kuwaandaa vijana kwa maisha ya baadaye kwa kuwawezesha wanafunzi hao kujiendeleza kimasomo kupitia zao hilo.

Ameongeza kuwa miche hiyo wanapewa wanafunzi hao bila malipo wakapande katika maeneo yao kwenye mashamba yao ama ya wazazi/ walezi wao na si kwenda kupanda mashamba au maeneo ya shule na kwamba kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza atapewa miche 10 na kuwataka waitunza ili iweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

"...nyie wanafunzi wa form one, tunataka kila mwanafunzi mmoja leo hii, tumuachie miche ya mikarafuu kumi... miche hii isiwe mali ya shule mkaipande kwenu..." amesisitiza Dkt. Mussa

Kwa mujibu wa Katibu Tawala huyo, kwa sasa bei ya kilo moja ya karafuu ni shilingi 20,000/= hivyo, mche mmoja una uwezo wa kuzalisha kilo tano huku akisema kuwa kwa miche hiyo 10 itazalisha kilo 50 ambazo ni sawa na shilingi 1,000,000/=  hivyo, kupitia zao hilo wanafunzi wataweza kujigharamia masomo yao kupitia zao la mkarafuu. 

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Morogoro Dkt. Rozaria Rwegasira amesema kapeni hiyo ilizinduliwa rasmi Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, na inaendelea kutekelezwa halmashauri zote za Mkoa huo na sasa wako Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, huku akiwataka wanafunzi kuipokea kampeni hiyo ambayo itawasaidia kutimiza ndoto zao.

Naye, Mwl. Isakwisa Asesisye akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero amemshukuru Katibu Tawala huyo kwa kuanzisha kampeni hiyo ndani ya Mkoa huo na sasa iko Mvomero Halmashauri yenye jumla ya shule za sekondari 37 ambapo kwa kuanzia kampeni hiyo imeanza kwa shule za Homboza na Kipera.

Nao Wanafunzi waliopatiwa miche hiyo wameeleza kufurahishwa na mpango huo, wakisema kuwa utapunguza changamoto za ada na mahitaji mengine kwao lakini pia kampeni hiyo itawajengea misingi ya kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea.

Jumla ya wanafunzi 473 wa shule za Sekondari ya Kipera na Homboza  wamepatiwa jumla ya miche 4730 ya karafuu.

Kampeni hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 17-02-2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ampapo takribani miche 9000 ya mikarafuu iligawiwa Kwa wanafunzi wa kidato Cha kwanza wa Shule za Sekondari za Tegetero, Tawa,Kinole,Mkuyuni, na Kiroka .
















Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.

Video zaidi






Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa








Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO A UPANGA VYUMBA VYA OFISI NA MAENEO MBALIMBALI YALIYOPO MOROGORO MJINI March 19, 2025
  • TANGAZO LA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU, DEREVA NA MTENDAJI WA KIJIJI July 15, 2024
  • TANGAZO LA RASIMU July 25, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi karibuni

  • KIONGOZI MBIO ZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI ILIYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 12, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEEA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO,MAAGIZO YATOLEWA

    April 11, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO AENDELEZA KAMPENI YA JISOMESHE NA MKARAFU

    March 14, 2025
  • "BAINISHENI VYANZO VYA MAJI NA MVILINDE" MHE.KASSIM MAJALIWA MAJALIWA

    March 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Mfumo wa Mikopo ya 10% Namna ya Kujisajili
Vidio Zaidi

Kurasa za haraka

  • Sheria ya Manunuzi ya umma
  • Sheria ya Ardhi

Tovuti nyingine

  • Salary Slip Self Service
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani yake

Wasiliana nasi

    Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road

    Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania

    Simu: +255 23 2935458

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.