VIKUNDI 62 VYA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU VYAPATIWA MAFUNZO YA MKOPO WA ASILIMIA KUMI.
Vikundi vya wajasiliamali Sitini na mbili(62) vilivyopitishwa na Kamati ya Uhakiki wa mikopo ya
Wilaya ya Morogoro, Leo Tarehe 19-06-2025 vimepatiwa mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha matumizi sahihi ya mkopo watakayopatiwa.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa divisheni ya kilimo Mifugo na Uvuvi Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mhandisi.Magreth Kavaro amewasisitiza wanavikundi kukumbuka kufanya marejesho Kwa wakati na kuweka kumbukumbu za miamala na taarifa za Kikundi huku akikazia na msemo wa "Mali bila daftari, hupotea bila Habari"
Mafunzo hayo yaliyotolewa na idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro yalijikita zaidi Katika Utunzaji wa Kumbukumbu na Ujazaji wa Mikataba.
Sambamba na mafunzo hayo wanavikundi walipatiwa mafunzo kuhusu utatuzi wa migogoro, mafunzo yaliyotolewa na mtaalamu wa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Ndugu Steven Maheri.
Pia elimu ya usalama barabarani ilitolewa Kwa wanavikundi Kwa kutambua ya kwamba vipo vikundi vilivyopatiwa mkopo ambavyo vinajishughulisha na Huduma ya kusafirisha abiria na mizigo Kwa kutumia pikipiki maarufi Bodaboda, elimu iliyotolewa na maafisa wa Jeshi la polisi kutoka Kata ya Mvuha.
Vikundi vyoye 63 vinatarajia kunufaika na mkopo wa thamani ya Shilingi milioni Mia Tano Thelathini na nane na Laki nne 538,400,000/= ambapo Vikundi vya Wanawake vitapata Shilingi 363,400,000/= Vijana Shilingi 163,000,00/= na Walemavu Shilingi 12,000,000/= .
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.