Jumla ya wanafunzi 7126 wa darasa la saba wanatarajia kufanya mtihani wakumaliza elimu ya msingi kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Katika mtihani huu unaotarajia kufanyika kote nchini kuanzia octoba 07 hadi 08 jumla ya wavulana 3558 na wasichana 3568 wanatarajia kufanya mtihani huukutoka katika shule 155 ambapo shule mbili niza binafsi na shule 153 nizaserikali kati ya shule 160 za msingi zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Wanafunzi ambao wanafanya mtihani huu ni wale walioingia darasa la kwanza mwaka 2014 ambapo jumla ya wanafunzi 7686 waliandikishwa, wavulana wakiwa 3856 na wasichana 3830.
Tayari maandalizi yote muhimu kwa ajili ya ufanyikaji wa mitihani huo ikiwemoupelekeji wa mitihani katika vituo teule vya kuhifadhia mitihani yameshafanyika.
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro inapenda kutoa wito kwa wazazi, na walezi wa wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani kuhakikisha wanawapatia watoto wao mahitaji muhimu yatakayowawezesha kufanya mtihani katika hali ya utulivu.
Witounatolewa kwa wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mtihani wa kumalizaelimu ya msingi kutojiusisha na mbinu zozote zile za udanganyifu wakatiwa kufanya mtihani ambazo zitapelekea kufutiwa matokeo yao.
Sambamba na hilo wasimamizi wa mitihani wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia kwakuzingatia sheria, kanuni na taratibu za mitihani pamoja na utumishi wa umma ila kuhakikisha mitihani inafanyika na kumalizika bila dosari yoyote.
Katika mtihani uliofanyika Mwaka 2019 jumla ya wanafunzi 7447 kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ambapo wavulana walikuwa 3656 na wasichana 3791 huku kiwango cha ufaulu kikiwani asilimia 53
Aidha,kwa mwaka 2020 Halmashauri ya wilaya ya Morogoro inatarajia kufaulisha kwazaidi ya asilimia 80.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.