Na. Tajiri Kihemba, MOROGORO DC.
Maafisa Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro leo februari 10, 2022 wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa Anwani za makazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali katika utambuzi wa watu na makazi kupitia mfumo wa Anwani za makazi na postikodi.
Mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Maafisa hao ni hatua ya awali ambapo hatua inayofata ni kutoa mafunzo kwa Maafisa Watendaji wa vijiji tayari kwa utekelezaji wa zoezi hilo la utambuzi wa mitaa, barabara na utoaji wa namba za nyumba.
Lengo la anwani za makazi ni kuanzisha mfumo sahili wa anwani ulio katika
muundo rahisi kuutumia katika kutoa majina ya barabara au mitaa, vitongoji
nambari za nyumba na hatimaye upangaji wa anwani kwa nyumba katika barabara au mtaa husika.
Manufaa ya Mfumo wa Anuani za Makazi;
* Kila mtu anayeishi Tanzania atakuwa na anwani halisi ya makazi.
* Kila biashara inayosajiliwa Tanzania itakuwa na anwani halisi ya makazi.
* Utambulisho wa watu wanaoishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utarahisishwa.
* Usajili wa mali, biashara, vizazi na vifo utaboreshwa.
* Huduma za dharura, kama vile polisi, zimamoto na magari ya wagonjwa,
zinaweza kutambua maeneo yenye dharura na kuyafikia kwa haraka.
* Wageni wanaweza kubaini mahali wanakokwenda kirahisi.
* Mabenki na taasisi nyingine za fedha zitaboresha utendaji kazi wao.
* Mamlaka za Mapato zitabaini walipa kodi kirahisi.
* Makampuni yanayotoa huduma kwa umma yataboresha huduma zao.
* Muda mfupi utatumika katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi ikiwa ni pamoja na usafiri na huduma za posta.
Zoezi hili kwa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro linatarajiwa kufanyika kwa haraka na kukamilika kabla ya tarehe 30.3.2022, Wananchi wote mnaombwa kutoa ushirikiano kwa Maafisa hao wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.