Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuanza mbio zake mkoani Morogoro kuanzia tarehe 21/7/2018 hadi tarehe 29/7/2018. Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kwa Mwaka huu ni Ndg Charles Kabeho kutoka mkoa wa Dar es Salaam akishirikiana na Bw. Issa Abasi Mohamed (Kusini Pemba), Bi. Agusta Safari (Geita), Bw. Ipyana Mlilo (Tanga), Bw. Dominick Njunwa (Kigoma) na Bi. Riziki Hassan Ali (Kusini Unguja).