Benki ya CRDB tawi la Morogoro Agency limefanya ziara ya upendo kwa kuwatembelea watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro iliyopo eneo la Mvuha leo hii tarehe 13/10/2020.
Ziara hiyo ambayo ni mikakati ya benki hiyo ya kuwa karibu na wateja wake ilifanyika katika wiki ya Huduma kwa wateja ambapo walitoa keki ya Upendo kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika ofisi za Halmashauri Mvuha Meneja wa Tawi la Morogoro Agency Bi Glory Mponzi aliyeambatana na Bwana Godfrey Pasweto walielezea umuhimu wa wiki hii ya huduma kwa wateja na pia kuishukuru Halmashauri ya Morogoro pamoja na watumishi kwa kuendelea kuwa wateja wa Benki hiyo.
Akiongea kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Morogoro Bi Florence Mwambene alitoa shukrani kwa uongozi wa Benki hiyo kwa kufika eneo la Mvuha siku hiyo na kushiriki pamoja katika tendo hilo la upendo na kuahidi kuwa Halmashauri itaendelea kushirikiana na Benki hiyo katika mipango mbalimbali ya maendeleo.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Postal Address: 1880, Morogoro Tanzania
Telephone: +255 23 2935458
Mobile:
Email: ded@morogorodc.go.tz
Copyright © 2017 Morogorodc. All rights reserved.