Mkurugenzi wa vijana ajira na watu wenye ulemavu Ndugu Juma Abrahamani ameeleza kuvutiwa na miradi ya Vijana na walemavu katika Halmashauri ya Morogoro. Akiwa katika ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana na wallemavu wilayani hapa Ndg Juma aliweza kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na vijana wilayani hapa.
Aliweza kutembelea mradi wa Kufyatua matofali eneo la Mvuha, Ghala la kuhifadhia nafaka kijiji cha Mbwade kata ya Bwakila chini, kutembelea eneo la uwekezaji la utalii Majimoto Kisaki.
Katika hotuba yake alielezea kuridhishwa na utekelezaji wa asilimia nne za vijana katika Halmashauri ya Morogoro na pia aliwasisitiza vijana kutunza mradi, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kurejesha fedha na wizara haitosita kuwasaidia katika kuboredsha mchakato wa kuongeza thamani katika miradi yao.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Postal Address: 1880, Morogoro Tanzania
Telephone: +255 23 2935458
Mobile:
Email: ded@morogorodc.go.tz
Copyright © 2017 Morogorodc. All rights reserved.