Na. Tajiri Kihemba, MOROGORO DC.
Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) imewasilisha taarifa yake ya mrejesho wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya katika Halmashari ya Wilaya ya Morogoro. Akiwasilisha taarifa hiyo Afisa TARURA, Ndugu Gebo Mlangwa amesema,
"Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro iliidhinishiwa bajeti ya matengenezo ya barabara ya thamani ya Tshs. 1,119,800,000.00 ambayo iliainishwa katika matengenezo ya barabara. Hata hivyo baadae TARURA halmashauri ya wilaya ya Morogoro ilipokea maelekezo ya ongezeko la bajeti Kiasi cha Tshs 1,500,000,000.00 kwa kila jimbo kufanya jumla ya ongezeko hilo kuwa Tshs 3,000,000,000.00 (bilioni 3) Pamoja na kupewa ongezeko hilo Ofisi ya TARURA ilipokea maelekezo ya kukutana na wabunge wa kila jimbo ili kupata vipaumbele vya kila jimbo ambavyo vitafanyiwa matengenezo kutumia fedha hizo."
Aidha mpaka sasa TARURA Halmashauri ya wilaya ya Morogoro imeshaingia mikataba Saba (7) kwa awamu ya kwanza yenye thamani ya Tshs 1,003,323,720.00 mingine iko katika hatua za manunuzi.
Akitoa taarifa ya miradi ya barabara inayotekelezwa katika Halmashari ya Wilaya ya Morogoro, Afisa kutoka TARURA, Ndugu Gebo Mlangwa amesema,
"Juhudi za Ufunguzi wa barabara mpya unaendelea kufanywa kwa kushirikisha wananchi wa vijijini na Taasisi mbalimbali ambao ni wadau wa miundo mbinu ya barabara. Halmashauri kupitia TARURA tunaendelea kutoa ushauri na utaalamu katika barabara mpya zinazofunguliwa na wananchi na kisha kuzipima na kuzisajiri katika mfumo wa kutunza kumbukumbu za barabara (District Roads Management System –DROMAS).
Mpaka sasa zaid ya km 60 za barabara tumeshazipima na zinasubiri hatua za usajiri na ofisi ya TARURA imeshapokea maombi ya kupima barabara nyingine kutoka Kata za TAWA, BWAKIRA CHINI, NGERENGERE, KISAKI, MVUHA,KIDUGALO, KIROKA,MATULI, KIBUNGO JUU, KIBUKO NA MKUYUNI tunatarajia kufanyia kazimaombi haya ya kupima barabara katika kipindi hiki cha kiangazi kati ya mwezi Agosti na Oktoba."
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.