UTALII KATIKA ENEO LA KISAKI MAJI MOTO
Mahali ilipo
Chemchem za majimoto zipo umbali wa kilomita 150 toka Morogoro mjini ikiwa ni moja ya vivutio vya utalii katika Wilaya ya Morogoro. Ni chemchemambazo zipo katika mazingira mazuri, asilia na hivyo kuwa kivutio kwa wageniwanaotembelea eneo hilo. Picha hapa chini inaonesha moja ya chemchem ikiwa imetengeneza umbile la creater. Sehemu ya katikati ni maji yanayochemka kama inavyoonekana katika picha:
Mwonekano wa chemchem ya maji moto- Kisaki hot springs
Shughuli zinazofanyika
Wageni wengi hupitia kwa ajili ya kupiga picha na kufurahia mandhari nzuri ikiwani uwanda wa nyasi zinazostahimili joto kali. Kunawa, kuoga na kuchemshamayai ni moja ya shughuli zinazopendelewa na wageni. Zipo imani zinazothibitisha maji hayo kutumika kutibu magonjwa ya ngozi pamoja na kuondoa mikosimbalimbali katika jamii.
Moja ya mgeni aliyetembelea kisaki Hotsprings
Fursa nyinginezo
Chemchem za maji moto zimepitiwa na njia kuu ziendazo hifadhi ya taifa ya Nyerere (Nyerere National Park), na Hifadhi ya taifa ya Mikumi (Mikumi National Park) ambapo wageni hutembelea kujionea urithi wa dunia.
Wanyamapori ni moja ya vivutio vya utalii
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.