UTALII KATIKA MSITU WA HIFADHI WA KIMBOZA
Mahali ulipo
Msitu wa hifadhi wa Kimboza upo umbali wa kilomita 45 toka Morogoro Mjini.Msitu umezungukwa na vijiji vinne (4) vya Mwarazi, Changa, Kibangile naKilemela. Makao makuu ya hifadhi ya msitu ni kitongoji cha Kibungo chinikilichopo kijiji cha Mwarazi. Ukubwa wa msitu ni hekta zipatazo 405.
Kibao elekezi cha Msitu wa Hifadhi Kimboza- eneo la Kibungo chini
Asili ya neno Kimboza
Limetokana na neno la kabila la Kiluguru “Hotza” ikiwa na maana ya kupozamatatizo mbalimbali yakiwemo magonjwa na njaa. Hii ilitokana na msitu huukunufaisha vijiji jirani kwa kuwa na miti ya dawa, ukindu, na uwepo wa vyanzovingi vya maji kwa matumizi mbalimbali. Mboga za asili mfano delega, mlendana uyoga vinapatikana katika msitu huu kwa matumizi ya nyumbani.Ndani ya msitu wa hifadhi kuna miti ya matunda ya asili (milimili) ikiwa nichakula cha binadamu pamoja na ndege. Matunda haya yanaiva kwa mafungu(bundles) kama yanavyoonekana katika picha hapa chini:
Matunda aina ya milimili yanayofaa kuliwa na binadamu
Michikichi (Palm trees) – Mimea hii ni ya asili na hutoa matundayanayotumika kutengeneza mafuta ya mawese. Mafuta haya husaidiakung’arisha macho kwa watu wenye uoni hafifu. Mbegu za michikichizimeenea katika tarafa ya Matombo ambapo wakazi wake hukamua mafuta nakuuza kwa lengo la kujipatia kipato.
Mafuta ya mawese yakiwa kwenye ujazo tofauti kwa ajili yakuuzwa
Aidha Michikichi ni moja ya mimea asilia iliyoota kwa wingi na kutengenezamwonekano mzuri ndani ya msitu sambamba na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Michikichi ikiwa ni moja ya uoto wa asili katika msitu waKimboza
Dawa za asili:
Zipo dawa za kutibu magonjwa mbalimbali ndani ya msitu yakiwemo magonjwa ya tumbo, Malaria, meno na kuongeza nguvu za kiume.
Wanyama Adimu
Katika msitu wa hifadhi wa kimboza kuna mjusi anayefahamika kwa jina maarufu Mjusi williamsi (Electric Blue Dwarf Gecko) na ambaye hapatikani sehemu nyingine duniani. Muda mzuri wa kumuona mjusi ni majira ya asubuhi kabla jua halijachomoza. Tofauti ya jike na dume ni kupitia rangi zao ambapo dume huwa na rangi ya blue na jike huwa na rangi ya kahawia kama wanavyoonekana katika picha hapa chini:
Mjusi Williams-Dume na Mjusi Williams-jike
Makazi ya mijusi ni kwenye mimea inayojulikana kwa jina la Kiswahili Mikongepori (Pandanus spp).
Baadhi ya Ndege wakiwemo hondohondo, njiwa na wanyama kama mbegaweusi na weupe, Dondoro, Mbawala, Funo na Nguruwe pori wanapatikanakatika msitu huu.Miti ya asili: miti ya asili yenye umri wa miaka 50 na zaidi inapatikana katika msitu wa hifadhi. Ipo mikangazi, mininga, mipululu, mivule na mininga maji
Pango la milango nane: Pango hili ni kivutio kwa kuwa na mfano wa milango yakuingilia, kutokea, sebule pamoja na vyumba vya kupumzika.
Moja ya mapango katika msitu wa hifadhi- Kimboza
Choka wahawi
Hili ni neno la kabila la waluguru ambapo eneo hili ni pango lililotumiwa nawazee wa kale kutoa adhabu kwa watu waliosadikiwa kuwa wachawi. Waliokirimakosa waliachiwa kwa sharti la kutokurudia tena kwa kula kiapo cha kimila.Eneo hili pia lilitumika kwa matambiko kwa kutumia mti ulioitwa Mtambika
Kibao elekezi ndani ya msitu wa hifadhi kuelekea maeneo yamatambiko
Dago la njiwa
Kwa maana ya pango la njiwa kwa lugha ya kiswahili ikiwa ni makazi ya njiwa na kanga. Ndege hawa huruka majira ya asubuhi kwenda kutafuta chakula na kurudi nyakati za jioni kwa ajili ya kulala.
Mtalii akiwa kwenye dago la njiwa
Ukanda wa Mimea vamizi: Ukifika msitu wa Hifadhi wa Kimboza utafanikiwakuona athari za mimea vamizi aina ya Misederea (Cedrela odorata) ikiwaimeshamiri na kuzuia kuota na kushamiri kwa miti ya asili (Allelopathic plants).Miti hii ina sifa ya kuwa na harufu kali inayozuia kushambuliwa na mchwa.
Miti aina ya misedera ikiwa imepukutisha majani
Vyanzo vya maji ya chumvi
Ndani ya msitu wa Hifadhi kuna vyanzo vingi vya maji kwa matumizi ya binadamuna viumbe hai wengine. Vijiji vinavyozunguka msitu wa hifadhi vinanufaika nauwepo wa maji safi na salama.
Moja ya chanzo cha maji kinachowanufaisha wananchi
Shughuli zinazofanyika
Safari za miguu kuanzia majira ya saa kumi na mbili asubuhi kwa lengo lakuona mijusi, ndege, wadudu na wanyama wengine. Kupiga picha namapumziko katika eneo maalum (camp sites) bila kuathiri mazingira ni moja yashughuli zinazofanyika katika msitu wa hifadhi.
Moja ya safari za miguu (Walking safari ) katika msitu wahifadhi - Kimboza
Moja ya banda la Mapumziko (Resting bandas) -Msitu wahifadhi kimboza
Muda mzuri wa kutembelea hifadhi: Kuanzia mwezi Mei hadi Septemba kwavile miezi iliyobaki ni ya mvua nyingi.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.