FURSA YA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UTALII
MSITU WA HIFADHI PANGAWE MASHARIKI NA MAGHARIBI
Mahali ulipoMsitu wa hifadhi Pangawe Mashariki na Magharibi upo km 15 kaskazini masharikimwa mji wa Morogoro kupitia barabara ya Morogoro –Mkuyuni. Miinuko katikahifadhi hii ni ya wastani japo kuna miinuko mikali katika eneo la mwinuko wa Bondwa (Bondwa hills).
Uoto wa asili
Uoto wa asili katika msitu wa hifadhi Pangawe mashariki na magharibi ni miti yaaina ya Miyombo (80%), misitu ya asili(15%) na nyasi fupi (5%). Mimea mingikatika hifadhi hii imetoweka kwa kasi kutokana na matumizi mbalimbali yakibinadamu. Miti mingi katika hifadhi hii imekuwa kivutio kwa matumizi na hivyokupelekea uvunaji haramu. Ipo miti kwa ajili ya mapambo, Mbao, Dawa za asili,nguzo, kamba,kuni, uzio, mkaa, kivuli,rangi za asili, matunda, maua yanyuki, sumu ya kuvulia samaki pamoja na nyuzi.Aina za Mimea: Katika utafiti wa mimea uliofanyika mwaka 2003, hifadhi hiiinasadikiwa kuwa na aina 90 za mimea ya aina mbalimbali na familia 30. Idadikubwa ikiwa miti aina ya miombo mfano Mitopetope, Misufi pori, Milama,Ming’ong’o . Kwa bahati mbaya miti hii mikubwa kwenye hifadh hii imetowekana kubaki miti midogo midogo na vichaka. Tafiti zaidi zinahitajika kujua sababu zakutoweka kwa kasi kwa mimea ya asili katika hifadhi hizi.
Miti jamii ya Miombo hifadhi ya mlima Pangawe
Vyanzo vya maji: Zipo chemchem chache katika hifadhi hii ambazo zinatiririshamaji wakati wa mvua na kukauka wakati wa kiangazi.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.