FURSA ZA UTALII KATIKA MSITU WA HIFADHI WA MILAWILILA
Mahali ulipoMsitu wa hifadhi wa Milawilila unapatikana kijiji cha Milawilila kata ya TawaTarafa ya Matombo umbali wa kilomita 13 toka barabara kuu ya Bigwa –Kisaki(kupitia Matombo Msalabani). Msitu huu unasimamiwa na vijiji viwili ambavyo niMilawilila na Mifulu kilichopo kata ya Tegetero.Asili ya jina la msitu: Jina la msitu Milawilila limetokana na mti uitwao“Mlawilila” ambao haupatikani sehemu nyingine duniani. Sehemu kubwa yamsitu wa hifadhi imetawaliwa na miti hiyo.
Kibao elekezi cha kuonesha msitu wa hifadhi wa Milawilila
Wakazi wa kijiji cha Milawilila ni wakulima na wafugaji. Mazao yanayolimwakwa wingi ni ndizi, mananasi, machungwa na machenza kwa ajili yabiashara. Aidha wanakijiji wengi wamehamasika kupanda miti ya mbao aina yaMisederea kwa ajili ya ujenzi. Msitu wa Milawilila unafikika kwa urahisi kwanjia ya barabara.
Barabara ya kuelekea msitu wa hifadhi na Utalii wa kilimo(Agrotourism)
Shughuli za utalii katika vijiji vinavyozunguka msitu wa kijiji cha Milawilila
Utalii wa mazao ya viungo:
Mazao ya viungo kama iliki, pilipili manga,Mdalasini, karafuu na tangawizi ni moja ya mazao ya biashara yanayostawi vizuri katika eneo hili. Aidha, wageni wanapata fursa ya kufahamu mimea halisi inayozalisha viungo, mfano miti ya mdalasini, pilipili manga, iliki, karafuu namingineyo.
Miti ya karafuu pamoja na karafuu iliyovunwa (Utalii kilimo) ikiwa inakaushwa kwamaandalizi ya kupelekwa sokoni.
Miti inayopatikana ndani ya msitu
Ipo miti ya asili ikiwemo misufipori,Milengolengo, Mivule, Mikalati, mikangazi pamoja na mitiki ambayoimepandwa mipakani. Miti aina ya mianzi (bamboo forest) yenye tabia yakutunza vyanzo vya maji inapatikana katika msitu huu.
Msitu wa Mianzi (Bamboo forest) unaohifadhi vyanzo vya maji Wanyama wanaopatikana msituni: Wapo Mbega weusi na weupe, tumbili,kima, vyura na nyoka wa aina mbalimbali.
Wanyama katika hifadhi ya msitu wa Milawilila
Matumizi ya msitu:
Kwa sehemu kubwa msitu unatumika kwa shughuli zakimila (matambiko) na hivyo kulindwa na wazee wa mila. Hali hii inafanya msitu ubaki katika hali ya uasilia ukilinda mimea na vyanzo vya maji kamaunavyoonekana katika picha.
Moja ya vyanzo vya maji katika msitu wa hifadhi Milawilila
Matumizi mengine ni tafiti za baioanuai kwa kupitia wataalamu toka vyuo vikuu.Wageni wanaotembelea msitu:
Msitu huu ni kivutio kikubwa kwa wasanii/waigizaji wanaopiga picha katika maeneo ya hifadhi asilia. Wageni wengine niwatafiti ambao mara nyingi wanapitia kijiji jirani cha Mifulu kilichopo kata yaTegetero kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuingia msituni.Muda wa kutembelea msituni: Muda mzuri wa kutembelea msituni ni kuanzia mwezi Mei hadi Septemba kwa vile kuanzia mwezi Oktoba hadi Aprili nimsimu wa mvua za vuli pamoja na masika.Shughuli za utalii zinazoweza kufanyika: Kuongoza wageni kupitia njia za miguu, kuona dawa za asili ndani ya msitu, kuona matunda yaasili,kutembelea maeneo ya matambiko, kusikiliza sauti za ndege nawanyama.
Safari za miguu ndani ya msitu wa hifadhi- Milawilila
Eneo la kuweka kambi (camping sites): Ndani ya msitu wa hifadhi yapomaeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuweka kambi (camp sites) kwa wageni wanaohitaji kupumzika.
Daraja la zege Mto Mvuha Daraja hili ni mpaka kati ya kijiji cha Milawilila na kijiji cha Mifulu kilichopo kataya Tegetero. Katika eneo hili watalii wanapata fursa ya kuona mipaka baina ya vijiji viwili. Daraja hili limerahisisha huduma ya mawasiliano baina ya vijiji viwili vinavyopakana na msitu.
Daraja linalotenganisha kijiji cha Milawilila (Tawa) na kjijicha Mifulu (Tegetero)
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.