WANAMICHEZO MKAHAMASISHE WANANCHI KUJITOKEZA KUPIGA KURA TAREHE 29 OKTOBA,2025". Mhe. DKt Batilda Buriani
Wanamichezo wametakiwa Kutekeleza kwa Vitendo kauli Mbiu ya Mashindano ya SHIMISEMITA yaliyotamatika Jijini Tanga inayosema
" Jitokeze Kupiga Kura kwa Maendeleo ya Michezo ".kwa kuhakikisha wanajitokeza Kushiriki kupiga Kura Tarehe 29 Oktoba 2025 na kuhamasisha Wananchi Kujitokeza kupiga Kura siku hiyo.
Hayo yamesemwa leo tarehe 29 Agosti 2025 na Mhe. DKt Batilda Buriani Mkuu wa Mkoa wa Tanga wakati akifunga Mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) Jijini Tanga ambapo aliwataka wanamichezo hao kuhakikisha wanaihamasisha jamii kupitia Michezo Ili wajitokeze kupiga Kura ifikapo Tarehe 29 Oktoba 2025.
"Tumieni Michezo kuhamasisha Umma kujitokeza Kushiriki kupiga Kura Tarehe 29 Oktoba,2025".Alisema Mhe. Batilda na kuongeza"Michezo hii ni Moja ya Fursa za kutangaza Halmashauri kwa Wananchi, kutambua ziko wapi na pia Watumishi kufahamiana kupitia Michezo". Alisisitiza Mhe. Batilda wna kuongeza
Jumla ya Halmashauri 150 kati ya 184 zimeshiriki Mashindano hayo ya SHIMISEMITA Jijini Tanga ambapo washiriki ni 3504 kati yao Wanaume 2114 na Wanawake 1390 wamecheza Michezo Mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu,Mpira Wa Pete, Kamba , Riadha, draft nk
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.