Serikali imewataka Wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha za kutosha kwaajili ya kitengo cha Michezo, Sanaa na Utamaduni ili watumishi waweze kushiri vyema katika shughuli za kimichezo kama Shimisemita.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Tamisemi Mh. Zainab Katimba wakati akifungua Mashindano ya Shimisemita, Mapema Leo Agost 23 2025 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga .
Mh. Naibu Waziri amewataka pia Watumishi na wanamichezo kutumia Mashindano hayo kama chachu ya Kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa Mwaka huu kama Kauli mbiu ya Shimisemita 2025 inavyosema “ JITOKEZE KUPIGA KURA KWA MAENDELEO YA MICHEZO. “
Aidha amewataka Wakurugenzi wasioleta watumishi wao katika Mashindano ya Shimisemita Jijini Tanga wahakikishe Wanaleta watumishi wao kabla ya muda wa kufungwa kwa Mashindano hayo.
Kufikia Leo Agost 23 2025 katika ufunguzi wa Shimisemita Jijini Tanga ni Halmashauri 150 pekee zilizoleta Timu za watumishi kati ya Halmashauri 184 , hivyo jumla ya Watumishi walioshiriki Mashindano ni 3504 ambapo Wanawake ni 1390 na Wanaume 2114
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.