Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Wilaya ya Morogoro Ndg Reuben Sanga amewataka wananchi wa Kisaki na maeneo jirani kutumia fursa ya uwepo wa kambi ya huduma ya afya zinazotolewa bure katika kituo cha Afya Kisaki kwa ushirikiano serikali na wadau.
Haya ameyazungumza mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Kisaki na kukuta huduma zinaendelea, ambapo huduma hizo zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 20/8/2025 kutamatika 22/8/2025.
"Imekuwa ni siku ya furaha kwetu, hili zoezi ni muhimu sana kwa afya zetu. Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wametuletea huduma za vipimo na tiba mbalimbali, kwa pamoja tuitumie fursa hii kufanya uchunguzi wa afya zetu, na ni vyema kuchangamkia fursa ya kupata vipimo ili tuweze kupambana na magonjwa katika ngazi ya chini kabisa" amesisitiza Bw. Reuben.
Nae Mratibu wa huduma za jamii Bi. Hellen Joram kutoka NOMAD-Taasisi inayojishughulisha na maswala ya utalii, amesema kwamba huduma wanazozitoa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii hasa zinazozunguka hifadhi za taifa na kwamba huduma hizo wanazitoa bure.
Huduma hizo ni pamoja huduma za macho na miwani, Uchunguzi wa fistula, na ulemavu kwa watoto unaotibika kwa njia ya upasuaji na ushauri wa Hali ya lishe hasa kwa watoto.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kisaki wameishukuru Serikali na wadau kwa kuwaletea huduma za afya tena zikiwa ni Bure.
Serikali imeendelea kusogeza huduma za mkoba kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro na viunga vyake na wananchi wanaendelea kunufaika na upatikanaji wa huduma hizo zinazohusisha uwepo wa madaktari bingwa
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.