HAKIKA TUMEPAMBANA TUMETOLEWA HATUA YA FAINALI
Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Riadha mbio za Kupokezana vijiti mita 400 ,na Riadha mita 200 Wanaume zimepambana na Kutolewa katika hatua ya Fainali.
Akizungumza na Wanariadha wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Afisa Kiongozi Michezo Sanaa na Utamaduni Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Ndg Anania Sama amewapongeza hatua waliofikia huku akiwataka wasikate tamaa kwani kufika Fainali Katika Halmashauri 150 zilizoshiriki ni jambo la kujivunia.
"Vijana wangu mmepambana lakini Katika mashindano yeyoye ni lazima Mshindi apatikane haikua bahati yetu, lakini kitendo Cha kufika hatua ya Fainali Katika Riadha iliyoshirikisha takribani Halmashauri 150 ni jambo la kujivunia" amesema Sama.
Katika Mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea Jijini Tanga Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imeshiriki Katika Michezo ya Karata na Bao ambapo washiriki wametolewa hatua ya 16 Bora, Mchezo wa Vishale wametolewa hatua ya Nusu fainali. Kutupa Tufe Wanawake nafasi ya 7 kati ya 12 walioshiriki.
Mashindano yanayotarajiwa kufika tamati 29-08-2025 yalianza Rasmi Tarehe 15 August 2025 Katika Viwanja Mbalimbali Jijini Tanga huku yakibeba Kauli mbiu ya
"Jitokeze kupiga kura Kwa Maendeleo ya Michezo"
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.