Mradi huu upo katika Kijiji cha Mkambarani Kata ya Mkambarani ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Ujenzi wa Mradi huu ulianza mwaka 2014, chini ya Kampuni ya Mihan gas inayojishughulisha na ujazaji na usambazaji wa Gas kwenye mitungi kwa ajili ya matumizi ya majumbani. Kampuni hii inatumia rangi ya njano na ina aina tatu za ujazo,ambayo ni mitungi ya kilogram 38, 15 na 6.
Lengo la Mradi huu ni kuhakikisha Gas kwa matumizi ya majumbani inapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu ili jamii iweze kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa kwa lengo la kuhifadhi Mazingira .
Hadi kufikia sasa mradi huu umegharimu jumla ya tshs 600,000,000/= ikiwa ni gharama za ujenzi , mitambo na umeme. Fedha zote ni za Kampuni.
Faida zitokanazo na kuwepo kwa mradi huu katika Halmashauri ya Morogoroni pamoja na; Kutoa ajira kwa jamii hasa vijana, Kusaidia uhifadhi wa Mazingira, Kusogeza huduma kwa wananchi pamoja na kuongeza kipato kwa Halmashauri.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.