Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15 Mei, 2021 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa pamoja na Watendaji wa Taasisi mbalimbali.
Katika uteuzi huo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Martin Reuben Shigella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akichukua nafasi ya Bw. Lengai Ole Sanare aliemaliza muda wake. Kabla ya Uteuzi huu, Bw. Martin Reuben Shigella alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Taarifa hiyo ya Uteuzi imetolewa na Bw. Garson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Karibu Morogoro Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.