Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro katika Tarafa ya Bwakila kata ya Bwakila na kijiji cha Bwakila Chini. Katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijijini hapo siku ya Jumapili tarehe 8/10/2017 Mkuu wa mkoa aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama mkoa, mkuu wa wilaya ya Morogoro pamoja na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya. Katika hotuba yake mkuu wa Mkoa alikemea udhalimu unaofanyiwa watu wenye walemavu wa ngozi (albino).
Dr. Kebwe alikemea pia tabia inayojirudiarudia ya mapigano kati wakulima na wafugaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Akisisitiza wote kuishi kwa Amani na upendo kwani wakulima na wafugaji wanantegemeana.
Katika Mkutano huo wa hadhara Mhe. Mkuu wa mkoa alisikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Na alitoa maagizo kadhaa kwa watendaji wa halmashauri katika kutatua kero za wananchi. Maagizo hayo ni pamoja na:-
Ofisi ya mkurugenzi kupitia idara ya Ardhi kuzungukia vijiji vyote vyenye migogoro ya ardhi na kuitafutia ufumbuzi.
Idara ya Maliasili katika ofii ya mkurugenzi wilaya Jumuiya hifadhi wayamapori wa jukumu
Aliwaagiza pia maafisa watendaji kata na vijijiji kuwajibishwa pindi matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa albino yatakapotendaka katika maeneo yao ya utawala.
Mkuu wa mkoa aliwaagiza pia watendaji wa vijiji kushughulikia suala la mifugo na wafugaji wavamizi katika maeneo yao
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.