Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo jana apokea zawadi mbalimbali kwa vituo vya afya vya Ngerengere na Duthumi. Zawadi hizo zimetolewa ikiwa ni katika mpango wa benki hiyo kurudisha faida kwa jamii pamoja na kutekeleza kwa vitendo katika kuunga mkono jitihadi za serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo.
Zawadi hizo ni pamoja na vitanda vya kuzalia vitatu, magodoro saba, mashuka 40 delivery set tatu na mackingtosh moja. Mkuu wa wilaya amewashukuru NMB kwa misaada mbalimbali wanayoendelea kuitoa kwa jamii ya wana Morogoro na kuwataka waendelee na moyo huo huo wa kujitoa kwa ajili ya taifa.
Akipokea zawadi hizo mkuu wa wilaya amewataka watumishi wa vituo vya afya na zahanati kuvitumia kwa umakini na kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kudumu zaidi.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.