JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAISI TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA MOROGORO
MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA HALMASHAURI YA WILAYA MOROGORO KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro inaendelea na maandalizi ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020. Kazi hii inafanywa na sekta zote ambapo kuna Idara 12 (Utumishi na Utawala, Fedha za Biashara, Mipango Takwimu na Ufuatiliaji, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Afya, Kilimo Umwagiliaji na Ushirika, Maendeleo ya Jamii, Mifugo na Uvuvi, Usafi na Mazingira na Ardhi na Maliasili) na Vitengo 6 (Nyuki, Manunuzi, Mkaguzi wa Ndani, Tehama, Sheria na Uchaguzi). Aidha Idara ya Maji haikuhusishwa katika maandalizi ya Bajeti hii kulingana na maelekezo kwamba Bajeti yake itaandaliwa na kuwasilishwa Wizara ya Maji.
Maandalizi haya yanafanyika kwa kuzingangatia mwongozo wa bajeti wa mwaka 2019/2020, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2015-2020), Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano, Mpango wa Taifa wa Maendeleo Endelevu, Miongozo mbalimbali ya Kisekta pamoja na Vipaumbele vya Wananchi.
Katika Bajeti hii, Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia Jumla ya Tsh. 42,625,824,024.50 ambapo kati ya kiasi hicho, Kiasi cha Tshs. 2,201,584,000.00 kitakusanywa kutoka Vyanzo vya ndani sawa na asilimia 5.2 ya Bajeti iliyopangwa.
Mchanganuo ni kama ilivyoainishwa kwenye jedwali lifuatalo:
NA.
|
CHANZO CHA FEDHA
|
KIASI
|
1
|
Mapato ya Ndani
|
2,201,584,000.00
|
2
|
Matumizi ya kawaida
|
2,037,091,850.00
|
3
|
Mishahahara
|
34,240,386,734.00
|
4
|
Miradi ya maendeleo
|
4,146,761,440.50
|
|
JUMLA KUU
|
42,625,824,024.50
|
Aidha Halmashauri inaendelea kuboresha wigo wa Bajeti iliyotolewa kadiri itakavyoendelea kupata maelekezo toka ngazi za juu hasa kupitia Wizara mama TAMISEMI.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.