Friday 27th, December 2024
@Morogoro Dc
Taarifa Ya Uchaguzi Mdogo Wa Madiwani Katika Kata Ya Kiroka Novemba, 2017
Utangulizi
Kata ya Kiroka ipo katika Jimbo la uchaguzi la Morogoro Kusini Mashariki katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Kata ya Kiroka ina jumla ya vituo vya kupigia Kura 26 vyenye wapigakura 6,295 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura la Mwaka 2015.
Uteuzi wa wagombea
Utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea zilianza kutolewa tarehe 20 oktoba 2017 hadi tarehe 26 Oktoba, 2017. Jumla ya vyama vya siasa vinne (4) vilichukua fomu za uteuzi. Vyama hivyo ni ACT, CCM, CHADEMA na CUF. Uteuzi wa wagombea ulifanyika tarehe 26 0ktoba 2017 ambapo wagombea watatu kutoka vyama vya siasa vitatu waliteuliwa, wagombea hao ni,
Mgombea wa chama cha ACT hakurudisha fomu.
Pingamizi za Wagombea
Pingamizi moja liliwasilishwa na Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo dhidi ya Mgombea wa Chama cha Mapinduzi kwamba Mgombea huyo wa CCM Bi Jamila Taji Mohamed Si Raia wa Tanzania na pia si mkazi wa kudumu wa Kata ya Kiroka.
Baada ya kupitia pingamizi hilo na kujiridhisha na nyaraka mbalimbali zikiwemo Kitambulisho cha Mpiga kura, Hati ya Kusafiria na Cheti cha kuzaliwa tulibaini kuwa pingamizi hilo halikuwa na msingi wowote kwa kuwa Ndg Jamila Taji Mohamed ni Raia wa Tanzania, na mkazi wa kudumu wa Kata ya Kiroka.
Hali ya Kampeni za Uchaguzi
Kampeni zilianza tarehe 27 Oktoba , na kumalizika tarehe 25 Novemba ,2017 ambapo kila chama kilifanya kampeni kwa umiliki wa kijiji kwa kila siku ya kampeni kwa kufuata ratiba iliyoratibiwa kwenye kikao cha pamoja na vyama vya siasa kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2017. Hata hivyo kulikuwa na ongezeko kubwa la wafuasi na viongozi wa vyama vya siasa kutoka nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikiwemo Mvomero, Gairo, Morogoro Manispaa na Tarime na kusababisha kuongeza nguvu za ulinzi wa Polisi wakati wa Kampeni.
]
Ukaguzi wa vituo vya kupigia kura
Ukaguzi wa vituo ulifanyika kwa kushirikiana na vyama vya siasa ambapo katika ukaguzi huo vituo vitatu vilivyokuwa kwenye nyumba za watu binafsi vilihamishwa kwenye maeneo ya wazi. Vituo hivyo ni Kimbwala, Milengwelengwe B na Temekelo B. Aidha, Vituo 10 vya muda vilijengwa ambavyo ni Mngozi, Ofisi ya Kitongoji Mwaya, Ofisi wa Kitongoji Kimbwala, Milengwelengwe A, Milengwelengwe B, Kisauke ofisi ya Kitongoji, Ofisi ya Kitongoji Temekelo ,Ofisi ya Kitongoji Temekelo B, Ofisi ya Kitongoji Temekelo C ,Tomondo juu na Njia panda ya Mikese.
Mafunzo kwa watendaji wa vituo vya kupigia kura
Mafunzo kwa Wasimamizi wa vituo ,Wasimamizi wasaidizi wa vituo na Makarani waongozaji yalifanyika kuanzia tarehe 23-25 Novemba, 2017 na kufuatiwa na ugawaji wa vifaa.Aidha viapo kwa watendaji wote wa uchaguzi na Mawakala wa vyama vya Siasa vilifanyika kwa mujibu wa Sheria.
Upigaji kura na matokeo ya Uchaguzi
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. Karatasi za kupigia kura na fomu mbalimbali zilikuwepo kwenye vituo vyote vya kupigia kura na kufanya upigaji kura ufanyike kwa wakati. Wapigakura 2,920 kati ya 6,295 (46.39%) walioandikishwa walijitokeza kupiga kura. Kura 51 (1.75%) ziliharibika, kura halali zilikuwa 2,869 (98.25%) ya kura zilizopigwa. Mgombea wa CHADEMA ndg Ngozoma Rahimu Ally alipata kura 277 (9.65%), mgombea wa CUF ndg Mbena Saimoni Jasters alipata kura 339 (11.82) na mgombea wa CCM Bi, Jamila Taji Mohamed alipata kura 2253 (78.53%). Hivyo, Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Mgombea wa CCM Bi, Jamila Taji Mohamedi alitangazwa kuwa Diwani wa Kata ya Kiroka. Matokeo ya uchaguzi kwa kila kituo yamewekwa kwenye Jedwali Na. 1. Nakala ya fomu namba 21C na 24C zimeambatanishwa,
Jedwali Na. 1: Matokeo ya uchaguzi kwa kituo cha kupigia kura
|
|||||||||
NA. |
KIJIJI |
JINA LA KITUO |
IDADI YA WALIOANDIKISHWA |
IDADI YA WALIOPIGA KURA |
IDADI YA KURA HALALI |
IDADI YA KURA HALALI KWA CHAMA |
ZILIZOHARIBIKA |
||
CCM |
CDM |
CUF |
|||||||
1 |
BAMBA
|
MSOWELO OFISI YA S/KIJIJI
|
91 |
70 |
68 |
50 |
17 |
1 |
2 |
2 |
BAMBA
|
OFISI YA KITONGOJI BAMBA A
|
182 |
86 |
86 |
84 |
1 |
1 |
0 |
3 |
BAMBA
|
OFISI YA KITONGOJI MNGOZI
|
77 |
33 |
33 |
31 |
1 |
1 |
0 |
4 |
BAMBA
|
SHULE YA MSINGI BAMBA
|
437 |
209 |
208 |
188 |
18 |
2 |
1 |
5 |
DIOVUVA
|
MSAMVU OFISI YA KITONGOJI
|
367 |
150 |
143 |
132 |
10 |
1 |
7 |
6 |
DIOVUVA
|
OFISI YA KITONGOJI MAHEMBE
|
228 |
103 |
103 |
81 |
22 |
0 |
0 |
7 |
DIOVUVA
|
OFISI YA KITONGOJI MSAMVU B
|
169 |
90 |
89 |
72 |
15 |
2 |
1 |
8 |
DIOVUVA
|
OFISI YA KITONGOJI MWAYA
|
95 |
49 |
49 |
45 |
4 |
0 |
0 |
9 |
DIOVUVA
|
SHULE YA MSINGI DIOVUVA
|
153 |
66 |
66 |
62 |
3 |
1 |
0 |
10 |
KIROKA
|
OFISI YA KITONGOJI BANZAYAGE
|
62 |
32 |
32 |
24 |
7 |
1 |
0 |
11 |
KIROKA
|
OFISI YA KITONGOJI KINGOGWE B
|
364 |
186 |
184 |
133 |
40 |
11 |
2 |
12 |
KIROKA
|
OFISI YA KITONGOJI TEMEKELO
|
470 |
236 |
234 |
205 |
27 |
2 |
2 |
13 |
KIROKA
|
OFISI YA KITONGOJI TETEMELO B
|
321 |
145 |
134 |
118 |
15 |
1 |
11 |
14 |
KIROKA
|
OFISI YA KITONGOJI TETEMELO C
|
438 |
208 |
203 |
173 |
28 |
2 |
5 |
15 |
KIROKA
|
OFISI YA MTENDAJI KATA KIROKA
|
302 |
146 |
146 |
104 |
32 |
10 |
0 |
16 |
KIROKA
|
OFISI YA S/KIJIJI KIROKA
|
375 |
181 |
179 |
143 |
28 |
8 |
2 |
17 |
KIROKA
|
SHULE YA MSINGI KIROKA
|
72 |
17 |
16 |
14 |
1 |
1 |
1 |
18 |
KIZIWA
|
KISAUKE OFISI YA S/KIJIJI
|
180 |
69 |
69 |
51 |
0 |
18 |
0 |
19 |
KIZIWA
|
MSOVIZI NJIA PANDA MIKESE
|
164 |
51 |
43 |
34 |
1 |
8 |
8 |
20 |
KIZIWA
|
OFISI YA KITONGOJI KIMBWALA
|
332 |
191 |
190 |
124 |
2 |
64 |
1 |
21 |
KIZIWA
|
OFISI YA KITONGOJI MILENGWELENGWE'A'
|
209 |
69 |
68 |
60 |
0 |
8 |
1 |
22 |
KIZIWA
|
OFISI YA KITONGOJI MILENGWELENGWE'B'
|
172 |
84 |
82 |
54 |
2 |
26 |
2 |
23 |
KIZIWA
|
OFISI YA S/KIJIJI KIZIWA 'A' -1
|
251 |
125 |
124 |
65 |
0 |
59 |
1 |
24 |
KIZIWA
|
OFISI YA S/KIJIJI KIZIWA 'A' -2
|
250 |
115 |
112 |
57 |
0 |
55 |
3 |
25 |
KIZIWA
|
SHULE YA MSINGI KIZIWA
|
311 |
128 |
128 |
79 |
3 |
46 |
0 |
26 |
KIZIWA
|
TOMONDO JUU OFISI YA S/KIJIJI
|
223 |
81 |
80 |
70 |
0 |
10 |
1 |
|
|
JUMLA |
6,295 |
2920 |
2869 |
2253 |
277 |
339 |
51 |
|
|
ASILIMIA |
|
46.39 |
98.25 |
78.53 |
9.65 |
11.82 |
1.75 |
Hali ya ulinzi na usalama
Vituo vyote vya kupigia kura vilisimamiwa na askari polisi mmoja kwa kila kituo,hata hivyo kulikuwa na askari 10 kwenye kituo cha kujumlishia kura na magari mawili ya Doria yenye jumla ya askari polisi 30 kabla ya siku ya kupiga kura, siku ya kupiga kura na baada ya kutangaza matokeo hali iliyopelekea Kata ya Kiroka kuwa na amani na utulivu kwa muda wote wa uchaguzi.
Changamoto
Zoezi hili lilikuwa na changamoto kubwa kwa wagombea kuteua mawakala toka maeneo mbalimbali ya Tanzania. Jambo hili liliwatia hofu wenyeji wa eneo husika na wakati mwingine kuzorotesha hali ya usalama. Ni muhimu kama ilivyo kwa wagombea, mawakala wawe ni wakazi wa eneo Kata au Jimbo linalofanya uchaguzi.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.