Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko Amemwagiza muwekezaji wa kiwanda cha marble cha Zhongfaa kufuata taratibu katika uendeshaji wa kiwanda chake na uchimbaji wa madini katika kijiji cha Maseyu kata ya Gwata wilayani Morogoro.
Muwekezaji huyu wa kiwanda cha Zongfaa anayoleseni ya kuendesha kiwanda cha Mable na hana leseni ya kuchimba madini/mawe ambayo ni malighafi katika utengenezaji wa mable hizo
“Wizara ya Madini tunapambana na Rushwa hatutaki urasimu, tunataka mwekezaji yeyote anayefuata utaratibu afurahie kuona kwanini amefuata utaratibu” alisisitiza Mhe Naibu waziri akiwataka wawekezaji wa sekta ya madini kufuata taratibu kwa kutokutoa rushwa katika suala zima la mchakato wa uchimbaji wa madini.
Aliwataka pia wananchi wa eneo la Kijiji cha maseyu kutoa ushirikiano kwa muwekezaji na kukuaa na vizuri ili wawekezaji waweze kusaidia upatikanaji wa maendeleo yao kwa haraka.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.