Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga amewataka Watendaji waafya katika Mikoa na Wilaya kusimamia matumizi ya fedha za Umma katika ngazizote na kukamilisha miradi ya zahanati, hospitali za wilaya na vituo vya afyaili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
MhandisiNyamhanga ametoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake katika Jiji la Mwanza naManispaa ya Ilemela na kukagua miradi ya maendeleo ambapo kwa upande wa afyaalikagua ujenzi wa kituo cha afya Igoma cha Jijini Mwanza na kituo cha afyaKarume na hospitali ya wilaya zote za Manispaa ya Ilemela.
“zingatienimatumizi ya fedha kwa kuwa na usimamizi makini katika ngazi zote na tumienimashine za kielektroniki kukusanya mapato ya Serikali, jengani majengo kwagharama nafuu yanayozingatia ubora unaotakiwa na kukamilisha ujenzi kwa wakatiili kuboresha huduma za afya kwa wananchi” alisema Mhandisi Nyamhanga
Aidha,Mhandisi Nyamhanga amesema mpaka hivi sasa katika sekta ya afya, Serikali imejenga jumla ya vituo vya afya 304 nchini kote na hospitali za wilaya 67ambazo zinaendelea kujengwa na kila hospitali mpya ya wilaya imekwisha pelekewa kiasi cha fedha shilingi bilioni moja na nusu.
Nyamhangaameagiza ujenzi wa hospitali mpya ya Manispaa ya Ilemela ijengwe kwa kufuataubora na kukamilika kwa wakati ili kufikia kufikia juni, 2019 ujenzi huo uweumekamilika kwa asilimia mia moja.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza Dkt. Juma Mfanga amesema kituo chaafya Igoma kimejengwa kwa kutumia nguvu za wananchi ambapo wamefanikiwa kujengamajengo sita ambayo ni jengo la upasuaji, jengo la wodi ya wazazi, jengo lamaabara, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la mionzi (x – ray) na jengo lakufulia nguo za wagonjwa.
Dkt.Mfanga amesema kukamilika kwa majengo ya kituo hicho licha ya kukabiliwa na changamotoya watumishi, tayari kimepunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali yawilaya ya Nyamagana, hospitali ya rufaa ya Sekou toure na hospitali ya rufaa yakanda Bugando mkoani Mwanza.
anaandika Fred Kibano
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.