Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Imeazimisha siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia katika viwanja vya Soweto vilivyopo katika kata ya Kiroka hapo jana tarehe 27/11/2019 kwa kufanya tamasha lililohudhuriwa na wananchi mbalimbali pamoja na wadau kama vile morogoro paralegal, TCRS, na USAID BORESHA AFYA ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Halmashauri Bi. Kibena Kingo.
Kila Novemba 25 hadi 10 Disemba ya kila mwaka ni siku 16 za kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia ambayo huadhimishwa kwa maandamano na kampeni mbalimbali kwa taasisi zinazojihusisha na masuala ya kuendeleza usawa wa kijinsia katika jamii.
Katika Mwaka huu kauli mbiu inasema "Hear Me Too" ikimaanisha nisikilize na mimi pia. Katika siku hizi 16 midahalo mbalimbali hufanyika ngazi ya Taifa, mkoa, wilaya pamoja na vikundi mbalimbali vya wanawake katika kuleta hamasa na kufikisha ujumbe kwa jamii kutokomeza vitendo vya ukatili kijinsia.
Katika maadhimisho hayo Shule za msingi na Sekondari, pamoja na vikundi vya Sanaa katika kata ya Kiroka zilizonyesha maigizo mbalimbali yenye ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia.
Ukatili wanaokumbana nao wanawake ni pamoja na kubakwa, kuombwa rushwa ya ngono, kunyanyaswa katika familia zao, kukeketwa na kunyimwa haki zao za msingi kama kwenda shule, kumiliki ardhi au kutoa maoni katika ngazi ya kifamilia na kijamii.
Hata hivyo, bado Serikali kwa shirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wanaendelea na juhudi za kutoa elimu na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaotekeleza ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha jamii inazingatia na kuheshimu haki za msingi kila mtu katika jamii.
Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro alitoa Zawadi kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi waliofanya vizuri. Pamoja na hayo mgeni rasmi aliwagawa wanafunzi wa kike wa sekondari taulo za kike.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.