Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imeadhimisha ya siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mvuha yalipo makao makuu ya Halmashauri iyo tarehe 01/12/2019 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Bi Rehema Bwasi. .
Katika maadhimisho hayo huduma mbalimbali za kiafya ziliweza kutolewa ikiwemo elimu juu ya virusi vya ukimwi, upimaji wa hiari, uchangiaji wa damu salama, upimaji wa saratani ya shingo pamoja na huma ya upimaji wa mlango wa kizazi.
Jumla ya watu 112 walijitokeza kupima virusi vya ukimwi ambapo wanawake walikuwa 30 na wanaume walikuwa 82.
Katika maadhimisho hayo michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa netball, riadha, kukimbia kwenye magunia, kukimbiza kuku, burudani ya ngoma zizlizobeba ujumbe wa ukimwi pamoja na maigizo na mashairi vilikuwepo.
Jamii ni chachu ya mabadiliko tuungane kupunguza maambukizi mapya
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.