Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro waliopo makao makuu Mvuha leo hii wamepata Elimu na uhabarisho wa afya juu ya kujikinga na ugonjwa hatari wa Korona. Elimu hiyo imetolewa na wataalamu wa idara ya afya katika Halmashauri ya wilaya wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya Bi Rehema Bwas pamoja na mganga mkuu Dr. Robert Mnyerere. Katika Mafunzo hayo watumishi wameaswa kuzingatia kanuni za afya kwa kunawa mikono wakati wote haswa ukizingatia kuwa watumishi wanahudumia watu mbalimbali wanaokuja kupata huduma katika makao makuu. Hii ni sehemu yauendelezaji wa kazi ya utoaji elimu juu ya Korona iliyoanza wilayani hapa hivi karibuni.
Imesisitizwa kuwa dalilli za ugonjwa wa Corona zionekanazo mara kwa Mara: ni pamoja na Homa, Kikohozi kibichi, Uhemaji wa tabu, Maumivu ya mwili, Kuuma kwa koo mfano wa matonses (tonsillitis), Kukosa hamu ya kula.
Dalili za mara chache za ugonjwa huu ni:• Kuhara, Kutapika, Kichwa kuuma, Kukohoa damu, Maumivu ya kifua
Watu wanaoweza kuzurika ni
• Watu wote (wakike kwa kiume) waweza kudhurika na korona
• Wenye maradhi yanayoshusha kinga mwili huwa na hatari kubwa Zaidi.
• Wazee pia wapo katika hatari kubwa kupatakorona kwani wana kingamwili hafifu.
KINGA:
• Kuosha mikono vizuri kwa maji safi na sabuni
• Tumia vikinga pua na mdomo (masks) ikiwa unahudumia washukiwa wa korona.
• Epuka kugusa na kurekebisha kikinga mdomo na pua (mask) na uso.
• Zingatia walau umbali wa futi 6 kutoka kwa mgonjwa mwenye korona
• Hakuna chanjo mpaka sasa
Kirusi cha korona katika mwili wa binadamu:
• Huchukua siku 2 mpaka 14 (wastani siku 5) kwa binadamu kuanza kuonesha dalili baada ya kuambukizwa na virusi vya korona (incubation perion)
• Huambukizwa kwa njia ya matone yatokanayo kwa kukohoa au kugusana moja kwa moja.
• Epuka kusalimiana kwa mikono
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.