Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema S. Bwasi amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi kutoka TRC na TFCG ambao wamejitoa kufadhili mradi wa Mkaa endelevu katika Kijiji cha Kinonko.
Kijiji cha Kinonko kimepitiwa na reli ya Kati pamoja na SGR hivyo TRC kwa kushirikiana na TFCG wameona wafadhili mradi wa Mkaa endelevu kijijini hapo katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kulinda Mazingira.
Bi. Rehema S. Bwasi amesema, "Tunawashukuru sana TRC na TFCG kwa kutuletea mradi wa Mkaa Mkaa endelevu katika Kijiji cha Kinonko kwa kuwa Mkaa endelevu una faida kubwa sana kwa Halmashauri yetu kwani kupitia mradi huu Wananchi wanakwenda kubadiri maisha yao na kuleta maendeleo ya Kijiji chao kama ilivyo katika Vijiji vingine vilivyowahi kufikiwa na mradi wa Mkaa endelevu, lakini pia mradi wowote ukifanyika huwa unaleta taswira nzuri kwa Halmashauri na Taifa kwa ujumla."
Akizungumzia jinsi mradi huo utakavyokwenda kufanikiwa, mwakilishi kutoka shirika la TFCG Bwana Emmanuel Lyimo amesema, "Kuna changamoto nyingi katika kufanikisha huu mradi wa Mkaa endelevu lakini kwa kushirikiana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Morogoro tutakwenda kufanikisha kwani tunaamini uwezo wao na uzoefu walionao katika kutekeleza miradi ya namna hii."
Mradi wa Mkaa endelevu ni mradi unaolenga kuwanufaisha Wananchi kupitia uchomaji wa mkaa pamoja na kulinda Mazingira.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Rehema S. Bwasi ameongeza kwa kusema kwamba amefarijika sana na amewahakikishia ushirikiano wa kutosha TRC na TFCG katika kufanikisha mradi huo katika Kijiji cha Kinonko na kuwaomba kama ikiwapendeza basi ifanyike na Vijiji vingine.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.