Leo tarehe 29/09/2021 timu ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro (CHMT) imefanya kikao chake cha kuweka mikakati juu ya utoaji Elimu na uhamasishaji Wananchi kupata Chanjo ya UVIKO-19 (Corona) kupitia kampeni maalumu itakayoanza tarehe 01/10/2021 kwa lengo la kuendelea kuwakinga Wananchi dhidi ya Ugonjwa huu hatari wa Corona.
Kikao hicho kilichoongozwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Dkt. Robert Manyerere kimekuja mara baada ya kumaliza kikao cha jana cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya kwa ajili ya kuweka mikakati ya utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando tarehe 29/09/2021.
Akifungua kikao hicho Dkt. Manyerere amesisitiza wajumbe wa kikao hicho kwenda kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa kuchanjwa na athari zitokanazo na kutochanjwa Chanjo ya UVIKO-19 ili Wananchi waelewe vizuri na kuachana na upotoshwaji unaotolewa na baadhi ya watu na sasa wapewe Elimu sahihi na hatimae wananchi waweze kuchanja kwa hiari yao.
Kikao hicho pia kilihusisha wadau wengine kutoka kutoka asasi za kidini, wazee maarufu na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kupata Elimu ya kutosha ili wakawe mabalozi wazuri kwenye kutoa elimu na kuhamasisha Wananchi kuchanjwa ili kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Wilaya ya Morogoro ipo katika kampeni yake maalumu ya utoaji Elimu na uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO-19 mtaa kwa mtaa kuanzia tarehe 01/10/2021 hadi tarehe 14/10/2021 kuhakikisha kila Mwananchi anaelewa vizuri kuhusu chanjo hii ya UVIKO-19 na hatimae wachanjwe kwa hiari yao.
#ujanjakuchanja
#chanjonihiari
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g #Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.