Na. Tajiri Kihemba, MOROGORO DC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi Rehema S. Bwasi leo Oktoba 25, 2021 amekutana na kufanya kikao na Wakuu wa Shule wa Shule zote zilizopata Mgao wa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, MVUHA.
Akifungua kikao kazi hicho, Bi Rehema S. Bwasi amewaambia Wakuu hao wa Shule Wakasimamie vyema ujenzi wa madarasa hayo na asitokee mtu wa kudokoa fedha hizo kwani ni za moto kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi Rehema S. Bwasi ameeleza Mgao huo na jinsi Halmashauri ilivyonufaika na mgao huo,
"Katika mgao wa fedha kupitia Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imenufaika kwa kupata madarasa 103 kwa ajili ya shule za Sekondari yenye thamani ya fedha za Kitanzania Bilioni 2 na Milioni 60, pia Halmashauri imepata mgao wa madarasa 11 kwa shule shikizi 5 za Msingi kwa thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 220, wakati huohuo Halmashauri imenufaika kwa mgao wa fedha kwa ajili ya kuanzisha huduma za dharula katika Hospitali ya Wilaya yenye thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 300 na nyumba ya watumishi wa Afya yenye thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 90 ambapo nyumba hiyo pamoja na jengo la dharula itajengwa katika eneo la Hospitali ya Wilaya", amesema Bi Rehema S. Bwasi.
Kikao kazi hicho kimehitishwa mahususi zaidi kwa ajili ya kuweka mikakati ya pamoja ya kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati ili kufikia Januari, 2022 wanafunzi wa kidato cha kwanza waweze kuyatumia.
#AsanteRaisSamiaSuluhuHassan
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.