Kamati ya fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro leo Novemba 2, 2021 imefanya Ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022.
Kamati hiyo imepongeza hatua iliyofikiwa ya Ukamilishwaji wa Zahanati ya Sesenga ambayo ilipatiwa fedha na Serikali kiasi cha Shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati hiyo pamoja na ujenzi wa Choo, kichomea taka pamoja na ujenzi wa nyumba ya Mganga wa Zahanati hiyo.
Kamati ya fedha, Utawala na mipango ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mhe. Hamisi Msangule licha ya kupongeza pia imeitaka kamati ya ujenzi kumalizia kabisa ujenzi wa choo, kichomea taka kwa haraka ili wataalamu wa Afya wapelekwe na Zahanati iweze kutoa huduma kwa Wananchi.
Kamati ya fedha, Utawala na Mipango itaendelea na Ziara yake hiyo kesho tarehe 3/11/2021 na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali.
#ZiaraKamatiyafedha
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.