Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Eng. Juma Chimwaga akikagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari Gwata leo Novemba 8, 2021.
Ujenzi huo wa vyumba vitatu vya madarasa uliotokana na mgao wa fedha kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan kupitia Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 unafanywa na Mkandalasi kutoka Jeshi la Magereza (Gereza la Mtego wa Simba).
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Mhandisi Juma Chimwaga amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi katika shule hiyo na kuwataka wakandalasi wengine wanaojenga katika maeneo mengine kuiga mfano huo ili kuweza kukamilisha ujenzi huo mapema mwanzoni mwa mwezi Desemba.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Gwata, Mhe Zongo Robe amesema wataendelea kushirikiana na Mkandalasi huyo na watahakikisha kazi inafanyika kwa kasi kubwa ziaidi ili waweze kukamilisha ujenzi huo mwanzoni mwa mwezi Desemba.
#AsanteRaisSamiaSuluhuHassan
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.