Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Dkt Robert Manyerere leo Novemba 10, 2021 ameongoza mazoezi ya viungo kwa watumishi na Wananchi wananchi wachache waliojitokeza katika kuadhimisha wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza.
Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza katika Halmashari ya Wilaya ya Morogoro imetoa fursa kwa watumishi wa Halmashauri pamoja na Wananchi kufanya mazoezi pamoja ikiwa ni moja ya njia ya kuepukana na Magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari (Diabetic Mellitus), Shinikizo la Damu (High blood Pressure), Ugonjwa wa Moyo (Heart Diseases), Uzito mkubwa kupita kiasi (Obesity) na kuwa na mafuta mengi mwilini (Dyslipidemia)
Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Dkt Robert Manyerere amewashauli watumishi na Wananchi wa Wilaya ya Morogoro kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
Watumishi hao pamoja na Wananchi pia wamepata nafasi ya kupima uzito na presha kwenye maadhimisho hayo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mvuha.
#MaadhimishoYaWikiYaMagonjwaYasiyoambukiza
#BadiliMtindoWaMaisha
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.