Na. Tajiri Kihemba, MOROGORO DC.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Albert Msando leo Septemba 11, 2021 ameshiliki kikao cha Baraza la Madiwani kupitia taarifa za Kata kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 katika Ukumbi wa Mikutano Pangawe, Morogoro.
Akitoa nasaha zake Mkuu wa Wilaya, Mhe Albert Msando amewataka Maafisa Watendaji wa Kata, Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri, utunzaji wa vyanzo vya maji na kusimamia Elimu na miundombinu yote ya elimu.
"Anaesimamia mapato yanayotokana na Kijiji husika ni Afisa Mtendaji wa Kijiji na kupeleka taarifa kwenye Kata hadi Halmashauri ya Wilaya, nawaagiza Maafisa Watendaji wa Kata taarifa zenu za Mapato zionekane kwenye taarifa hizi za robo." Amesema Mhe. Albert Msando.
Mhe. Albert Msando ameongeza kwa kusema kuwa kila mkuu wa Idara ana wajibu wa kukusanya mapato ya Halmashauri,
"Dt (Mwekahazina wa Halmashauri) sio Mkusanya mapato ni msimamizi wa mapato, Afisa Kilimo unatakiwa kuhakikisha mapato yatokanayo na Kilimo yanapatikana, Mwanasheria unahusika na faini zote za uvunjwaji wa Sheria kwenye mapato." Amesema Mhe. Albert Msando.
Kwa upande wa Elimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Albert Msando amesema kuwa pamoja na kusimamia ujenzi wa madarasa bado Maafisa Watendaji na Madiwani wakasimamie vizuri ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi kwenye Kata zao ikiwa pamoja na kuzuia mimba zilizokithiri kwa watoto.
Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Albert Msando amesema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro itaendelea kutoa ushirikiano kwa Maafisa Watendaji, Wakuu wa Idara na Waheshimiwa Madiwani ili kuweza kutekeleza majukumu vizuri.
#Barazalamadiwanikupitiataarifazakata
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.