Na Tajiri Kihemba, MOROGORO DC.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Albert Msando (@mkuuwawilayamorogoro ) ametoa agizo la kukamilika kwa zoezi la mfumo wa anuani za makazi hadi kufikia Machi 30 mwaka huu 2022.
Mhe. Albert Msando ametoa maagizo hayo kwenye Mkutano wa Baraza la ushauri la Wilaya (DCC) la kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2020/2021 na 2021/2022 hadi Disemba pamoja na mapendekezo ya Mpango wa bajati kwa mwaka 2022/2023, Mkutano huo ulifanyika jana Februari 8, 2022.
Serikali imeanzisha mfumo wa anuani za makazi kwa lengo la kuwa na mfumo sahili wa anwani ulio katika muundo rahisi kuutumia katika kutoa majina ya barabara au mitaa, vitongoji nambari za nyumba na hatimaye upangaji wa anwani kwa nyumba katika
barabara au mtaa husika.
Manufaa ya Mfumo wa Anuani za Makazi;
Kila mtu anayeishi Tanzania atakuwa na anwani halisi ya makazi;
Kila biashara inayosajiliwa Tanzania itakuwa na anwani halisi ya makazi;
Utambulisho wa watu wanaoishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
utarahisishwa;
Usajili wa mali, biashara, vizazi na vifo utaboreshwa;
Huduma za dharura, kama vile polisi, zimamoto na magari ya wagonjwa,
zinaweza kutambua maeneo yenye dharura na kuyafikia kwa haraka;
Wageni wanaweza kubaini mahali wanakokwenda kirahisi;
Mabenki na taasisi nyingine za fedha zitaboresha utendaji kazi wao;
Mamlaka za Mapato zitabaini walipa kodi kirahisi;
Makampuni yanayotoa huduma kwa umma yataboresha huduma zao;
Muda mfupi utatumika katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi ikiwa ni
pamoja na usafiri na huduma za posta.
Hivyo kila Mwananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Tanzania kwa ujumla wake mnaombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Serikali katika kufanikisha mfumo huu.
#morodcmpya #tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.