Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg Daniel Chongolo, akiwa katika ziara ya siku mbili (tarehe 3-4februari 2023) katika Halimashauri ya Wilaya ya Morogoro akikagua baadhi ya miradi inayotekelezwa ikiwemo jengo la hospital ya wilaya, ofisi ya CCM wilaya,jengo la ofisi za halmashauri hiyo,zahanati ya Mikese na shule ya bweni Ngerengere.
Pamoja na changamoto alizozibaini ameagiza madiwani,wataalamu na watendaji wa halmashauri kuwajibika na kutumia rasilimali vizuri kwa manufaa ya wananchi wa halmashauri hiyo.
Alipokuwa wilayani humo Ndg. Chongolo alipata wasaa wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ikiwa ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara,umeme,afya na maji.
Kwa baadhi ya changamoto aliziagiza mamlaka husika kama vile TARURA(barabara), RUWASA(maji), TANESCO(umeme) na Mkurugenzi wa Halmashauri kuzishughulikia huku akiwaahidi wananchi kuzichukua baadhi ya changamoto na kwenda kuzishughulikia.
Aidha ameagiza wakandarasi waliopewa miradi mbalimbali wazingatie muda na ubora wa utekelezaji wa miradi wanayopewa na serikali.
Katibu mkuu aliwasihi wazazi kuwasomesha watoto wao hasa watoto wa kike na wazazi kuacha dhana ya kusema mtoto wa kike hana haki ya Kwenda shule na hatimae kuwacheza na kuwaozesha mapema.
”Tabia hiyo iishe mara moja kwani Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassani anapambana na kuhakikisha madarasa yenye viwango yanapatikana na ametoa fedha nyingi katika sekta ya elimu”. Amesema Chongolo.
Katibu chongolo akiongea na wananchi wa Kijiji cha kinole alipokuwa kwenye ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
Katibibu mkuu wa CCM Ndug Daniel Chongolo akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Kiroka kuhusu changamoto zinazo wakabili Pamoja na kujua uhai wa chama hicho
Hata hivyo Chongolo amesema kuwa hataacha kuwauliza Wataalam Na Watendaji mbalimbali katika ziara zake kuhusu maendeleo ya miradi inayotekelezwa kwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha inaisha kwa wakati na wananchi wanapatiwa huduma stahiki kupitia miradi hiyo.
Katika ziara aliyofanya Ndg Chongolo amekuwa akitembea na watendaji pamoja na wataalam wa halmashauri kwa ajili ya kutolea majibu ya papo kwa hapo kwa wananchi kuhusu kero na changamoto zinazowakumba wananchi hao.
Ndugu Chongolo alikutana na changamoto ya upatikanaji wa maji baridi(yasiyo na chumvi) katika Kijiji cha Ngerengere na kumtaka mkurugenzi wa maji vijiji (RUWASA) na Bonde Wami Ruvu kuangalia namna watakavyoweza kufikisha maji katika Kijiji hicho kupitia mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya bilioni mbili (Mradi wa morong’anya hadi kinongo) au kutoka mto Mvuha.
Pia Ndg Chongolo amezungumzia ujenzi wa barabara itakayojengwa kwa kiwango cha lami itokayo Bigwa mpaka Kisaki ambapo hatua za awali zimeshaanza, ikiwa ni kutangaza zabuni. Na pia aliongelea ujenzi wa barabara kutoa ubena zomozi mpaka katika Kijiji cha ngerengere zabuni zimefunguliwa na kufikia mwezi wa nne katibu ameagiza mkandarasi waweameanza kazi. ‘’Na muwaajiri vijana wa hapa…. Nanyinyi nendeni VETA mkajifunze kuendesha mashine ya ‘scavetta’,uchomeleaji na taaluma nyingine’’.
Mbali na hayo Ndug Chongolo amewataka vijana kuachana na dhana ya kuishi Maisha ya kubahatisha na hatimaye kuanza kuchukua hatua kwa kujifunza fani tofauti tofauti pindi fursa zinapokuja wao ndiyo wawe wakwanza kunufaika na miradi itakayopelekea wao kupata ajira za muda na hatimaye za kudumu na kupunguza wimbi la vijana wengi kukaa vijiweni na kuacha kubeti ‘’maisha hayana bahati nasibu,Maisha ni bidi na kujituma’’ alisema Chongolo
Pia amewataka madiwani kuzungumzia kero za wananchi na kuacha kuzozana wenyewe kwa wenyewe bali kufanya kazi waliyotumwa na wananchi wao katika kata zao kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri ili kuleta maendelea kwa wananchi.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.