Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Rehema S. Bwasi leo Mei 18, 2022 amezindua kampeni na zoezi la utoaji chanjo ya Polio kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano.
Uzinduzi huo umefanyika katika Zahanati ya Mvuha katika Kijiji cha Mvuha ambapo kampeni hii sasa imeanza rasmi kwa wataalamu wa Afya kupita nyumba kwa nyumba kutoa Chanjo hiyo kwa watoto wa umri huo wa chini ya miaka mitano ili kuwakinga dhidi ya Ugonjwa huu wa Polio unasababisha kupooza kwa viungo vya mwili.
Akizungumza na Wananchi waliofika kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Rehema S. Bwasi amewataka Wananchi kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe @samia_suluhu_hassan katika kujali afya za Wananchi wake ndio maana sasa ameleta chanjo hii ya Polio baada ya Ugonjwa huu kuonekana katika Nchi jirani zinazopakana na Nchi yetu Tanzania.
"Nawaomba tujitokeze kwa wingi ili watoto wetu wapate chanjo hii ili kuwakinga na ugonjwa huu wa Polio unaosababisha kupooza, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda sana wananchi wake na ndio maana ameweka juhudi kubwa kuboresha sekta ya afya na kwa Halmashauri yetu ya Morogoro tumepokea fedha nyingi kwa ajili ya kujenga Vituo vya Afya, Zahanati, wodi za wanawake na wanaume, jengo la huduma za dharura, jengo la upasuaji wanawake na wanaume bila kusahau nyumba za watumishi wa afya ili waweze kutoa huduma za Afya kwa uhakika." Amesema Bi. Rehema Bwasi.
Katika hatua nyingine, Mlezi wa Timu ya wilaya ya uendeshaji wa huduma za afya (CHMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bi. Neema Shanalingigwa amewataka Wananchi hao kuipokea chanjo ya Polio na kuhakikisha watoto wote wanapata Chanjo hiyo.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Dkt. Robert Manyerere amesema Kampeni hii imeanza rasmi baada ya Mkurugenzi Mtendaji Bi. Rehema S. Bwasi kuzindua na itafanyika nyumba kwa nyumba watoto wote wafikiwe.
Kutokana na Nchi jirani kuripoti kuwepo kwa ugonjwa huu, Serikali ya Tanzania imeamua kutoa Chanjo ya Polio ili kuwakinga watoto wote.
#TuwakingeDhidiYaPolio #SENSA_AGOSTI23
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.