Mkurugenzi wa miundombinu kutoka wizara ya mifugo Eng.GODFREY MLOWE amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi miwili mikubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro katika kijiji chaa Kongwa na Magogoni vilivyopo katika tarafa ya Mvuha.
Lengo kubwa la ziara hiyo ni kukagua eneo ambalo litachimbwa bwana la maji (LAMBO) kwa ajili ya wafugaji katika Kijiji cha Kongwa na kukagua jengo ambalo litatumika kama kituo cha kukusanyia maziwa kutoka kwa wafugaji wa Halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imetengewa kiasi cha Tsh 442,537,760.00 na serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya ujenzi wa Lambo katika kijiji cha Kongwa inayotarajiwa kuanza mapema kuanzia sasa.
Pia Tsh 101,736,436.00 kwa ajili ya Kituo Cha Kukusanyia Maziwa ambapo ujenzi unaendelea na sasa ni hatua ya boma.
Akiambatana na Mkandarasi ndugu Mirogena, pamoja na baadhi ya wakuu wa idara wakiwemo idara ya Mifugo, injinia wa wilaya pia baadhi ya wananchi wa Kongwa, Eng. Mlawa walipata fursa ya kukagua eneo linalotarajiwa kuchimbwa Lambo hilo na kuwataka wananchi na uongozi kuonesha ushirikiano katika kipindi cha ujenzi mpaka ukamilifu wake.
Bwana Muselem, kwa niaba ya wananchi ameishukuru serikali kwa kuweza kusikiliza kilio chao ambapo ameahidi yeye na jamii inayozunguka eneo la mradi watautunza na kutunza mazingira kwa ujumla.
" Sisi kama wafugaji tunapenda kuishukuru serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuitikia ahadi na kuitekeleza ahadi iliyokuwa imeahidiwa wakati Waziri wa Mifugo alipotutembelea mwaka jana" alisema Ndg Muselem.
Hata hivyo Eng.GODFREY MLOWE amesema "mradi huo wa bwawa la maji utawanufaisha wafugaji katika nyakati tofauti kwani bwawa hilo litavuna maji mengi ambayo yatatosheleza kwa wananchi wote wa kijiji hicho"
Nae Eng. Juma Zahoro kutoka ofisi za Makao makuu ya halmashauri hiyo akiwa na Bi. Glory Malata ambaye ni afisa mifugo, kwa niaba ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika kuhikisha lengo la serikali kwa wananchi wa Morogoro linafikiwa hususani hili la miradi hiyo miwili iliyopo katika Tarafa ya Mvuha.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.