Vijana katika kijiji cha Pangawe wamenufaika kutokana elimu ya ushonaji vya mradi wa vyerehani uliopo kjijini hapo. Mradi huo una lengo kuu la kuwajengea vijana uwezo wa ujiajiri kupitia mafunzo ya ufundi ya ushonaji ili kuweza kujitegemea na kupambana na umaskini.
Mradi wa huu wa Kituo cha Ufundi cha Vijana upo katika kijiji cha Pangawe Kata ya Mkambarani. ulianzishwa chini ya ufadhili wa Shirika la Korea liitwalo Koica na kusimamiwa na Voluntia wa Korea kuanzia Oktoba 2010 kikiwa na wanachama 20 ambao ni Vijana wa kike,Kikundi hiki kinajishughulisha na shughuli za ushonaji wa nguo.Mradi huu ulikabidhiwa rasmi kutoka kwa Voluntia wa Korea tarehe 27 oktoba 2015 na sasa unaendeshwa na wanakikundi.
Kikundi kinamiliki jengo lenye vyumba viwili na vyerehani 25 vinavyotumiwa na wanakikundi katika shughuli ushonaji na kutoa mafunzo kwa wanafunzi.Tangu kuanzishwa kwa kikundi jumla ya wanafunzi 126 wamepata mafunzo ya ushonaji wa nguo na kujiajiri wenyewe.
Mradi huu mpaka sasa umegharimu jumla ya tshs, 5,630,000.00 ikiwa ni fedha ya vitendea kazi ,ambapo Wahisani walichangia 4,630,000/= na wanakikundi walichangia 1,000,000/=
Hadi sasa jumla ya wanafunzi 126 wamepata mafunzo ya ushonaji na kuwawezesha kujiajiri kupitia ushonaji na hivyo kujiongezea kipato
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.