Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kiroka Wilayani Morogoro baadaya mgombea wake Bi Jamila Taji Mohamed kuibuka kidedea kwa kuvishinda chama cha Chadema, pamoja na CUF katika uchaguzi uliofanyika jana tarehe 26/11/2017 na matokeo yaliyotangazwa jana usiku.
CCM iliibuka mshindi katika uchaguzi huo uliotokana na kiti hicho kuwa wazi baada yaaliyekuwa diwani wa kata hiyo Ndugu Robert Selasela kuteuliwa na Mhe Raisi kuwa, kuwa katibu tawala wilaya ya Ulanga.
Msimamizi wa uchaguzi katika kata hiyo Ndugu Safia Kingwai alimtangaza mgombea wa CCM, Jamila Taji Mohamed kuwa mshindi wa udiwani katika kata hiyo kwa kupata kura 2253 dhidi ya wapinzani wake Ndg Ngozoma Rahimu Ally wa CHADEMA aliyepata kura 277 wa NA Ndugu Mbena Justice Simoni wa CUF aliyepata kura 339.
Jumla kura zilizopigwa 2920 sawa asilimia 46.39 ya wale wote waliojiandikisha katika daftari kudumu kwa kata hiyo mwaka 2015.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.