Mnufaika wa mpango wa Kunusuru kaya maskini wilayani Morogoro, katika kijiji cha Changa kitongoji cha Sangasanga, Bi Nuru Abdallah ID no. 14 ameishukuru Serikali kwa mpango huo kuwa ni mzuri na wenye manufaa.
Akizungumzia mpango huo anasema kuwa umemnufaisha na kufanya maisha yake kuwa na ahueni tofauti na zamani huku akiwa na mifugo kadhaa ya mbuzi na kuku.
Bi Nuru ambaye ni mjane mwenye watoto wawali, amesema kuwa kupitia mpango wa Tasafu ameweza kumsomesha mtoto wake wa kwanza Tausi Mohamed hadi kidato cha nne. Na sasa anaendelea na masomo katika chuo cha ufundi Kibwaya. Pia bado anaendelea kumsomesha binti yake mwingine Samida Mohamed Shomari ambaye yupo Darasa la Saba katika shule ya msingi Changa.
Bi Nuru amefanikiwa kujenga nyumba yake ya vyumba vitatu na sebule na maisha yake yameboreke kwa kiasi kikubwa
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.