Taasisi isiyo ya kiserikali nchini Tanzania ECLAT kwa kushirikiana na Upendo Association ya nchini Ujerumani leo tarehe 15.02.2025 wamekabidhi madarasa matatu mapya, matatu yaliyokarabatiwa, matundu 32 ya choo ,16 upande wa wavulana na 16 upande wa wasichana, jiko la muda la kisasa, simtanki 2 zenye ujazo wa lita 5000 kwa kila moja yakiwa yameunganishwa kuweza kusambaza maji vyooni na jikoni mradi uliogharimu £100,000 mpaka kukamilika.
Mradi huu uliotambulika kwa jina la Kichangani School Project pia umewezesha kununuliwa kwa jumla ya madawati 137, viti vya ofisi 8 pamoja na meza za ofisi 8 vilivyokabidhiwa kwa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro halfa iliyofanyika shule ya msingi Kichangani kata ya Bwakira juu.
Akipokea makabidhiano hayo Afisa Taaluma elimu ya msingi Bi Idda Kitwana amewashukuru sana wafadhili hawa (ECLAT na Upendo Association) chini ya mwavuli wa FLY AND HELP iliyofadhiliwa na Christine Nicolai na kuahidi kukuza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa Shule ya msingi Kichangani kwani mazingira yameboreshwa na kuwa rafiki kwa kujifunzia.
"Niwaombe wanananchi na wakazi wote wa Kichangani Kisaki kuitumia fursa hii kuwahimiza watoto kusoma kwa bidii na kuyatunza mazingira ili yatufae kwa kizazi hiki na kizazi kijacho kwa maendeleo ya elimu". Amesisitiza Bi. Kitwana.
Aidha amewapongeza na kuwataka wahisani kuendelea kuboresha mazingira ya shule mbalimbali zilizopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi waalimu ili kuendelea kuwasaidia kusogeza huduma bora na za msingi kwa wananchi na kukuza kiwango cha ufaulu haswa kwa wasichana.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.