Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro leo Disemba 10 imefanya Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kihalmashauri yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bwakira Chini. Ikiongozwa na kauli mbiu: WEKEZA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA.
Akiongea kwa niaba ya mgeni rasmi Bi. Florence Mwambene amewataka wananchi wote kuzingatia mafunzo na mijadala mbalimbali iliyofanyika katika maeneo tofauti ya Halmashauri hiyo Toka siku ya uzinduzi 25, Novemba, 2023) mpk kufikia Leo siku ya 16 ambayo ndio maadhimisho.
Aidha vikundi mbalimbali vimeshiriki Kwa kutoa burudani,jumbe.na zawadi ikiwemo taulo za kike, juisi na biskuti Kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bwakira Chini na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Bwakira Chini.
Wadau mbalimbali wameshiriki wakiwemo TGNP, Kikundi Cha Wamasai, CAMA (CAMFED TZ), Wanawake na Maendeleo group,Baraka na Faraja.
Aidha Bi. Mwambene aliwataka wananchi kuendelea kupambana na rushwa, kuwa na maadiki kwani ni Moja ya mambo yanayoepusha matendo ya ukatili.
"Hivi Kuna mtu ataenda kumvizia mtu sijui pale kwenye mbuyu kama ana maadiki!? Kwa hiyo tuendelee kuhimizana maadili kuanzia kwenye familia zetu, shuleni, kwenye dini zetu na Kila pahala. Lakini pia kukemea vitendo vya rushwa" alisema Bi. Mwambene
Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia hufanyika Kila mwaka kuanzia tarehe 25, Novemba Hadi tarehe 26, Disemba, ambapo Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imehitimishia Leo 10, Disemba 2023 katika viwanja vya shule ya msingi Bwakira Chini.
KAULI MBIU:
"WEKEZA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA"
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.