Na. Tajiri Kihemba, MOROGORO DC.
Pamoja na changamoto ya kijiographia kwa Halmashauri yetu ya Wilaya ya Morogoro, bado Mkurugenzi inabidi tuhangaike kuhakikisha kwamba vituo hivi vya Afya vinakamilika kwa wakati ndani ya mwaka huu wa fedha 2021/2022.
Hayo yamesemwa Aprili 28, 2022 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mhe. Lukas J. Lemomo alipokuwa akifunga Mkutano wa Baraza la Madiwani kupitia taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Halmashari kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 kuanzia Januari hadi Aprili 2022.
Mhe. Lemomo amesisitiza ukamilishaji wa Vituo hivyo vya Afya viwili vipya vinavyojengwa Mkulazi na Kasanga ambavyo ujenzi wake unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali kuu jumla ya shilingi milioni 500 kwa vituo vyote viwili.
Pia Mhe. Lemomo amesisitiza ukamilishaji wa ujenzi wa shule mbili mpya za Sekondari zinazojengwa katika Kata za Kibuko na Bungu ambazo serikali imetoa fedha kiasi cha Shilingi milioni 470 kwa kila shule na kufanya jumla ya shilingi milioni 940 kwa ujenzi wa shule zote mbili.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Lukas J. Lemomo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema S. Bwasi kwa kuhakikisha watumishi wawili kutoka Idara ya Elimu makao makuu ya Halmashauri wanakuwepo kila siku katika eneo la ujenzi wa shule hizo mbili ili kusimamia maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo.
Naye Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ndugu Hilary Sagala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe Albert Msando amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Wakuu wa idara kuhakikisha wanafanya uhamasishaji kwa Wananchi kuhusu zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Tarehe 23/8/2022 Nchi nzima.
#SENSA_AGOSTI23
#morodcmpya #tunatekelezakwakasiya5g #kaziiendelee
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.