Timu ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro imeiagiza timu ya wataalamu (menejimenti) ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kuimarisha usimamizi wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashari ya Wilaya ya Morogoro.
Timu hiyo imeagiza hayo leo Septemba 17, 2021 ilipokuwa inaendelea na ziara yake ya Siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za Serikali na kuitaka Halmashauri kuongeza nguvu katika ufuatiliaji katika maeneo ambayo Serikali imepeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo ya Afya na Elimu.
Akizungumza mara baada ya kukamilisha Ziara hiyo, Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Rozalia G.R amesema Halmashari inatakiwa kujipanga na kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ili kuleta ufanisi na umaliziwaji wa miradi hiyo kwa wakati na thamani ya fedha iweze kuonekana.
Katika hatua nyingine Timu hiyo ya ufuatiliaji imepongeza ujenzi wa mradi wa Maabara ya shule ya Sekondari Matombo.
"Tumetembelea ujenzi wa maabara mbili za physics na chemistry ambapo walipewa Million 30 kwa ajili ya kukamilisha maabara hizo mbili, kwa kweli tumeangalia, tumetembelea kila mahali na tumeridhishwa na jinsi walivyofanya ukarabati na umaliziaji wa hizo maabara mbili kwa ufanisi mzuri na zinapendeza na zipo vizuri kutumika." Amesema Katibu Tawala Msaidizi - Uchumi na Uzalishaji, Dkt. Rozalia G.R
"Kuna mapungufu madogo tumeyaona kwa mfano kwenye ile mifereji sehemu ambazo hawajaziba waweze kuziba, lakini kwa mambo mengine Maabara ipo vizuri kwa hapa shule ya Sekondari Matombo." Ameongezea Dkt. Rozalia G.R
Timu hiyo ya Ufuatiliaji imefanikiwa kukagua miradi 12 ikiwemo majengo ya Shule ya Msingi Mdokonyole, Sekondari ya Kisaki, Zahanati ya Lubasazi, Sekondari ya Mvuha, Hospitali ya Wilaya, Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.