Ikiwa imebaki siku 1 tu kuzinduliwa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la mpiga kura Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, ambapo kitaifa zoezi hili litafanyika kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma na Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania,
Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro wameendelea kuhimizwa na kuhamasishwa kupitia msanii maarufu nchini ndugu Rashidi Mwinshehe maarufu kama 'Kingwendu' kuanzia siku ya kesho kufika kushiriki zoezi la uandikishaji. "Wakazi wa Mvuha mambo vipiii...Naomba ndugu zangu kuanzia kesho mpaka tarehe 20 uende ukajiandikishe ili ikifika tarehe 27 Novemba umchague yule umpendae kwa raha zakoo". Haya yamezungumzwa na msanii Kingwendu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa shule ya msingi Mvuha saa 11:30 jioni akitokea kata za Mikese, Tununguo na Ngerengere katika zoezi zima la uhamasishaji wa uandikishaji wa wapigakura katika daftari la mpiga kura kwa serikali za mitaa 2024.
Tumuunge mkono mh. Raisi kwa kujitokeza kwa wingi katika vitongoji vyetu kujiandikisha ili kupata tiketi ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27, Novemba 2024.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.